Kongamano la Miiraji Tarehe 25/05/2014 saa 2:00 asubuhi Ukumbi wa CCM Mkoa - Arusha. More... Click Here!


About Us


بسم الله الرحمن الرحيم 


UWASUWA ni umoja wa walimu wa  kiislamu ujulikanao kwa jina  Umoja wa walimu wa Ahlis-Sunna Waljamaa  (Shafy),
Umoja huu utafanya  kazi Tanzania  nzima  kwa kuanzia  mkoani Arusha ambapo mako makuu yake  yatakua  mkoani Arusha.
Umoja huu haufungamani na Serikali, usiokuwa wa  kutengeneza faida  na usiofungamana  na itikadi yoyote ya kisiasa.

MALENGO NA MADHUMUNI.

Malengo na madhumuni ya umoja huu yatakua  haya yafuatayo:-


1. Kuanzisha, Kusimamia na Kuendeleza Madrasa  na vyuo vya elimu ya mwongozo  na mazingira  kwa Waislamu  na kuinua viwango vya Elimu kwa wanafunzi na Walimu wa Kiislamu.


2. Kusimamia na kutetea  haki za msingi  za walimu wa madrasa  na jamii ya kiislamu kwa ujumla.


3. Kutafsiri na kuandika  vitabu, majarida , vipeperushi na maandishi mengine  kwa ajili ya kufikisha elimu ya dini ya Kiislamu kwa jamii ya Kiislamu.


4. Kuanzisha na kuhimiza daawa (Tabligh ) ya din ya Kiislamu 


5. Kusimamia malezi na maadili mema kwa vijana wa Kiislamu na Waislamu kwa ujumla.


6. Kuanzisha na kuendeleza uhusiano mzuri kati ya umoja na taasisi nyingine  za Alhis- sunna waljamaa.


7. Kuanzisha miradi na shughuli za uchumi na uzalishaji mali kwa ajili ya kupiga vita umaskini.


8. Kulinda kutetea na kuendeleza itikadi ya Ahlis-Sunna waljamaa kama vile  kuadhimisha kuzaliwa mtume  Muhammad ( S.A.W) sherehe ya mwaka mpya wa Kiislamu, ,Khitma , Talqini………………………N.k


9. Kufanya michango mbalimbali kwa nia  ya kuimarisha  na kuendeleza madhumuni na malengo yaliyotajwa ya umoja huu.

10. Kufanya jambo lolote lisilo nje ya sheria kwa ajili ya kuimarisha na kuendeleza madhumuni na malengo yaliotajwa ya umoja huu pamoja na kuinua uchumi wa umoja kwa ujumla

 



 



0 comments:

Post a Comment

Copyright @ 2014 UWASUWA.

Designed by Japhary | Japhary Juma