Kongamano la Miiraji Tarehe 25/05/2014 saa 2:00 asubuhi Ukumbi wa CCM Mkoa - Arusha. More... Click Here!


Thursday, 20 June 2024

UMOJA WA WALIMU MKOA WA ARUSHA UNAENDELEA KUPANGA SAFU YAKE VIZURI

USTADHI ABUBAKAR BIN ALLY AKIWA KATIKA USIMAMIZI WA SHUGHULI ZA KIDINI JIJINI ARUSHA -TAREHE 20/6/2024 HABARI KAMILI KESHO IJUMAA KABLA YA ALASIR
 

Sunday, 15 October 2023

UMOJA WA WALIMU WA MADRASA MKOA WA ARUSHA

 MGAWANYO WA BAADHI YA MAJUKUMU.

ILI KAZI ZIWE NYEPESI NA KILA MWANA UMOJA AWAJIBIKE KATIKA NAFASI YAKE UMOJA ULIGAWA MAJUKUMU YAKE KATIKA IDARA ZIFUATAZO :-                                                             

    1- IDARA YA UTAWALA

    2- IDARA YA USAJILI

    3- IDARA YA DA`AWA

    4- IDARA YA TAALUMA

    5- IDARA FEDHA NA UCHUMI.


SIKU BAADA YA SIKU TUTAENDELEA KUKULETEA KIUFUPI KAZI MBALI MBALI NA LALENGO YA UMOJA HUU KWA MASLAHI MAPANA YA UISLAMU NA JAMII KWA UJUMLA


Wednesday, 11 September 2019

MAULIDI MAKUBWA YALIYO ANDALIWA NA MADRASAT SHAMSIL MAARIF MRARA KISIWANI SIKU YA JUMAPILI TAREHE 8/9/2019

MADRASA HII IKO MKOA WA MANYARA MAENEO YA MRARA IKISIMAMIWA NA MWALIMU HAWADH KHAMISI AKISAIDIANA NA TIMU MAALUMU ALIYO IPANGA
MGENI RASMI SHEIKH WA MKOA WA MANYARA  SHEIKH MUHAMMAD KADIDI AKIWAWA PAMOJA NA SHEIKH WA WILAYA SHEIKH JUMA BIN SAID ISERE WALIZIDI KUIPAMBA HADHARA HIYO KWA KUJALI NA KUTHAMINI MWALIKO HUO
MZEE KHAMIS MUHAMMAD IKOME AKIWA NA SWAHIBA WAKE MZEE MUHAMMAD SELEMAN MWAHU WAKIWA NA  VILEMBA VYA VYEKUNDU WAKIWA WAMEKAA MEZA KUU
USTADH AWADH KHAMIS AKIFURAHIYA KASWIDA ILIYO KUWA IKIIMBWA NA MADRASA KUTOKA ARUSHA
JUKWAA LA KINAMAMA
JUKWAA LA WANAFUNZI UPANDE WA WASICHANA 
MADRASA MBALIMBALI ZILIHUDHURIA  KWA LENGO LA KUFANIKISHA HADARA HIYO

FUNDI MITAMBO NAE HAKUCHEZA MBALI NA MITAMBO YAKE 


Monday, 13 May 2019

UFUNGUZI WA SWALA YA IJUMAA KATIKA MSIKITI WA DAARULUL MUSTWAFA MANISPAA YA ARUSHA KATA YA TERATI MATAA WA BONDENI


MWANZO TULIKUWA KWENYE TURUBAI KAMA MSIKITI HUU UNAVYO ONEKANA, HATIMAYE TUKAWA TUMEPIGA HATUA NA KUWA KWENYE BATI KAMA UNAVYO ONEKANA HAPO CHINI NA TUNAMUOMBA ALLAH ATUPE SUBIRA NA NGUVU ILI MSIKITI HUU UFANANE NA MSIKITI MINGINE AMBAYO INAPIGA HATUA ZA KIMAENDELEO SIKU BAADA YA SIKU. POPOTE PALIPO NA MUHISANI ASIYE KUWA NA MASHARTI MAGUMU WA KUTUTIA NGUVU KWA AJILI YA MAENDELEO YA MSIKITI HUU ANAWEZA KUWASILIANA NASI KWANAMBA  ZIFUATAZO 0754040941 MWENYEKITI UWASUWA AU 0783366505 MUWEKA HAZINA UWASUWA AU 0783377149 IMAMU WA MSIKITI HUU
KINAMAMA WAKIWA WAMEJIBANA KATIKA MSIKITI HUO WAKITAFAKARI LINI NUSRA YA ALLAH ITAKUJA ILI WAWEZE KUSWALI KWA KUJINAFASI KAMA WAUMINI WA MAENEO MENGINE HUKU WAKIJIPA MATUMAINI KUWA BORA KIDOGO KULIKO KUKOSA KABISA
NAO KINA BABA WAKIKUNJA KUNJA MIKEKA YAO KWA HUZUNI MSIMU HUU WA MVUA KUTOKANA NA UDOGO WA MSIKITI HUO HUKU WAKTAFAKARI WAPI WATAPATA NGUVU ZA KUUPANUA MSIKITI WAO
KATIBU NA MWANAHARAKATI WA MSKITI HUO AKIWA NA BASHASHA HUKU AKISALIMIANA NA MUUMINI MWENZAKE SIKU YA UFUNGUZI WA SWALA YA IJUMAA BAADA YA KURUHUSIWA KUFUNGUA IJUMAA NA SHEIKH WA MTAA HUO SHEIKH AYOUB DENGU


HAO NI BAADHI YA WAUMINI WA MASJID DARUL MUSTWAFA KATIKA JIJI LA ARUSHA KATA YA TERATI MTAA WA BONDENI
USTADH MASOUD HUSSEIN AKIELEZEA KITU KWA WAUMINI HAO SIKU YA UFUNGUZI HUO ILIHALI BAADHI YA WAUMINI WANAMSIKILIZIA KWA NJE KUTOKANA NA UDOGO WA MSIKITI HUO
 
KINAMAMA WAKIWA NA MABINTI ZAO WADOGO SIKU YA UFUNGUZI WA SWALA YA IJUMAA

Wednesday, 16 January 2019

MAULIDI YA KINAMAMA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 20/1/2019 HAPO MASJID TAQWA MAJENGO

MWENYEKITI IDARA YA DA`AWA ( UWASUWA )USTADHI MIRAJI KHAMISI ANAWAALIKA KINAMAMA PAMOJA NA MABINTI  WA JIJINI ARUSHA KWENYE MAULIDI YA KUMUADHIMISHA MTUME MUHAMMAD (S.A.W) YATAKAYO SOMWA KESHOKUTWA JUMAPILI ASUBUHI KUANZIA SAA 3:00 NA KUENDELEA KARIBUNI MADRASAT TAQWA MAJENGO YA JUU

MADA MBALIMBALI ZITATOLEWA SIKU HIYO NA WAHADHIRI MBALIMBALI WAKIONGOZWA NA SHEIKH WA MKOA WA MANYARA SHEIKH MUHAMMAD KADIDI NA MWENYEJI WAO MUDIRI WA MADARASATI TAQWA USTADH KHALID MUSTWAFA
KARIBUNI SANA

Saturday, 27 October 2018

ZIYARA YA UWASUWA MKOANI MANYARA TAREHE 26/10/2018



 UMOJA WA WALIMU WATUA MKOANI MANYARA , ZIYARA KWA LENGO LA KUENDELEA KUFIKISHA UJUMBE WA MWENYEZI  MUNGU PIA KUBADILISHANA MAWAZO NA WAUMINI WA MAENEO HUSIKA  HUSUSAN  VIONGOZI WA DINI KWAHAKIKA KATIKA ZIYARA HIZO AMBAZO ZIMEDUMU KWA MUDA MREFU HUWA WAKAKUTANA NA CHANGAMOTO NYINGI SANA NA BAADHI YA CHANGAMOTO KUWEZA KUZIPATIA UFUMBUZI HAPO MANYARA WALIWEZA KUTEMBELEA MISIKITI YA MAGUGU,SINAI,BABATI MJINI NA ANGONI.
MADA MBALIMBALI ZILIWASILISHWA AMBAPO USTADHI ATHUMAN HUSSEIN KUTOKA MADRASA YA NURI NGARENARO YEYE ALIWASILISHA MADA KATIKA MSIKITI WA BONDENI HAPO MAGUGU ,MSIKITI WA SINAI MADA ILIWASILISHWA NA USTADH MASOUD HUSSEIN KUTOKA SHAMSIL MAARIF,BLOCO S MADA ILIWASILISHWA NA USTADH JUMANNE ALLY KUTOKA RAHMAAN NJIRO,MASJIDI RAHMA MADA ILIWASILISHWA NA USTADHI ISSA WA MASJIDI AQSWA MAJENGO YA CHINI,MASJID TAQWA MADA ILIWASILISHWA NA USTADHI MIRAJ KHAMIS WA MADRASAT TAQWA MAJENGO YA JUU NA USTADHI HABIBU WA MAENEO YA DAMPO MJINI ARUSHA YEYE ALIWASILISHA MADA YAKE KATIKA MSIKITI WA ANGONI C 

MSIKITI WENEYE HISTORIA KWA SHEIKH WA SASA WA MKOA WA MANYARA AMABAPO MWENYEJI WETU IMAMU WA MSIKITI HUU SHEIKH ABUBAKAR ALIWEZA KUTUSIMULIA KUWA MSIKITI HUO NI WA SIKU NYINGI NA  ASILI YAKE ULIKUWA NI UMEZEKWA NYASI NA ULIKUWA WA WA TOPE AMBAPO IMAMU WAKE WA KWANZA NA MWALIMU WA MADARSA ALIKUWA NI SHEIKH WETU WA MKOA SHEIKH MUHAMMAD KHAMIS KADIDI TUNA MSHUKURU SANA MUNGU MSIKITI WETU UNAZIDI KUPIGA HATUA ZA KIMAENDELEO KADRI SIKU ZINAVYO ZIDI KUSOGEA


HUU NI MSIKITI  KATIKA MAENEO YA SINAI AMBAPO UWASUWA WALIWEZA KUJIFUNZA MENGI KATIKA MSIKITI HUO KUTOKA  KWA USITADHI WA MADRASA YA KHAYRIYA USTADH ISSA PAMOJA NA KATIBU WA MSIKITI HUO ALLAH ALIPE KILA LAKHERI 

 USTADHI ISSA AKIWA OFISINI KWAKE AKIRATIBU BAADHI YA MAMBO  
MADRSAT KHAYRIYA MUONEKANO WAKE KWA NDANI

 BAADA YA ZIYARA HIYO USAFIRI WANAO UTUMIA UWASUWA ULIPITA KILA KITUO NA KUWAKUSANYA WANAUWASUWA KWAAJILI YA KURUDI MJINI ARUSHA KWA AJILI YA KUENDELEA NA MAJUKUMU YAO YA KILA SIKU


Monday, 15 October 2018

SEMINA YA WALIMU WA MADRASA KATA YA NAMANGA WILAYA YA LONGIDO

USTADHI SHAHIRAN SALUMU NASSORO AKIWA AMEVAA JAKETI LENYE MISTARI MIKONONI,AKIFUATIWA NA MENEYEKITI WA KATA YA NAMANGA MZEE ABUU A.ZUBERI,ANAYE FUATA NI MWALIMU ABUBAKAR MAMBOLEO WA MADRASA YA ISTIQAAMAH MTAA WA FIDOFOSI JIJINI ARUSHA,ANAYE FUATA AMBAYE ANAYE PERUZI SIMU YAKE NI SHEIKH RAMADAHAN MPANGALA SHEIKH (W) NAMANGA ANAYE FUATA NI MWL.TWAHA MOHAMED MPERA MWENYEKITI USAJILI UWASUWA ,ANAYEFUATA NI AMIM MUHIDIN RASHID ALIYE VAA SHATI LA DRARFT MWALIMU WA AL-HIDAYA ANAYEFUATA NI MZEE ALLY KASSU MWENEYE NDEVU NEUPE ,ANAYEFUATA MWENYE SUALI YA JINZI NI MWENYEKITI HALMASHAURI BAKWATA KATA YA LONGIDO NAWAMWISHO KABISA NI MWALIMU NASSORO HASSAN NASSORO MWALIMU WA MADRASA YA AL-HIDAYA ILIYOPO NAMANGA   .

WAWEZESHAJI WALIJIKITA ZAIDI KATIKA KUELEZEA MSHIKAMANO WA WALIMU KATIKA MAENEO YAO,NAMNA YA UTOAJI WA TAALUMA BORA NA DONDOO ZA MADARASA MBALIMBALI AMBAPO MWENYEKITI IDARA YA DA`AWA USTADHI MIRAJI KHAMIS ISSA ALIELEZEA UMOJA,USTADH TWAHA MOHAMED ALIELEZEA TAALUMA , USTADHI ABUBAKARI MAMBOLEO ALIELEZEZEA USHIRIKI NA NAFASI YA WAZAZI KATIKA MADRASA NA USTADH MASOUD HUSSEIN ALIELEZEA DONDOO ZA MADRASA .

WANASEMINA WENGI WALIPONGEZA SANA UMOJA WA WALIMU KWA SEMINA HIYO NAWENGI WALIKUWA NA SHAUKU YA KUJIUNGA KATIKA UMOJA HUO, WALIDADISI KWA KINA TARATIBU ZA UMOJA HUO NA ZAIDI WALIVUTIWA SANA PALE WALIPO SOMEWA KATIBA YA UMOJA KATIKA SURA YA PILI UKURASA WA KWANZA INAYOELEZEA MALENGO NA MADHUMUNI YA UMOJA HUO.
SEMINA AMBAYO ILIANZA MAJIRA YA SAA 5:00 ASUBUHI NA KUMALIZIKA SAA 9:30 ALASIRI BAADA YA SEMINA HIYO LILI TOLEWA TANGAZO KUHUSU MUHADHARA MKUBWA AMBAO UNATARAJIWA HKUFANYIKA JUMAPILI IJAYO PANAPO MAJALIWA YA M.MUNGU KUANZIA SAA 8:00 MCHANANA KUMALIZIKA SAA 12:JIONI HAPO NAMANGA .

NA HATIMAE SHEIKH MPANGALA ALIWASHUKURU SANA UMOJA WA WALIMU NA KUAHIDI KUWA WILAYA YAKE IKO TAYARI KUTOA USHIRIKIANO WA HALI NA MALI KATIKA KUPELEKA MBELE GURUDUMU HILI LA UMOJA PIA ALIPATA FURSA YA KUTANGAZA TANGAZO LA MHESHIMIWA MUFTI WA TANZANIA LINALOWAHUSU WAFUNGISHAJI NDOA KUWA MUFTI ANAWATAKA WAJISAJILI ONLINE .



Copyright @ 2014 UWASUWA.

Designed by Japhary | Japhary Juma