Mwezi wa shawwali ni mwezi ambao waislamu wote wasio kuwa na Udhuru wa kisheria wanahimizwa Kufunga siku sita ( 6 ) ambapo mwenye Kufunga Kwa kufuatanisha au kutofautisha muhimu Tu afunge siku hizo kabla ya mwezi huu kuisha .
Mtume Muhammad (s.a.w) amesema :Mwenye Kufunga Ramadhan Kisha akafuatishia sita katika mwezi wa shawwali anakuwa kama aliefunga mwaka mzima.
Wapendwa waislamu Hali ikiwa ni kama hivyo nawahimiza kila mmoja ajitahidi kabla ya mwezi kuisha apate siku sita za Kufunga Allah atuwezeshe na atusamehe makosa yetu
Aamiyn

