Kongamano la Miiraji Tarehe 25/05/2014 saa 2:00 asubuhi Ukumbi wa CCM Mkoa - Arusha. More... Click Here!


Monday, 26 May 2014

Filled Under:

KATIBU WA UWASUWA USTADH HUSSEIN HASSAN AKISOMA RISALA


UMOJA WA WALIMU WA AHLIS-SUNNA WAL JAMAA-ARUSHA
(UWASUWA)
RISALA FUPI KWA MGENI RASMI
Awali ya yote tunamshukuru M.Mungu kwa kutupa uzima tukaweza kuungana pamoja katika hafla hii.
Pili ,tunakushukuru mgeni rasmi kwa kuitikia mwito wetu pamoja na kuwa una shughuli nyingi na ni kipindi cha mapumziko (weekend).
HISTORIA FUPI YA UMOJA WA WALIMU
Umoja huu ulianzishwa mwezi march 2011 kwa malengo ya kuwaunganisha wanataaluma wa Dini ya kiislaamu katika Mkoa wa Arusha na nje ya Mkoa ili watekeleze majukumu yao katika jamii.
MAFANIKIO
1-Kwa uwezo wa M.Mungu umoja huu umenunua Ardhi yenye ukubwa wa mita 100x50 kwa ajili ya shughuli za kitaaluma na huduma nyingine za kijamii.
2-Umoja umekamilisha rasimu ya katiba yake na hivi sasa tuko kwenye mchakato wa kuanza kusajili.
3-Umoja umeziunganisha Madrasa,Walimu,Masheikh,na Viongozi mbali mbali wa Dini katika mkoa.
4-Umoja leo hii utazindua blog yake ijulikanayo kwa jina la uwasuwa.blogspot.com ambayo itasheheni mambo mengi yahusuyo umoja na hasa akida ya ahlus sunna waljamaa.
5-Umoja unajitahidi kuijenga jamii ya kitanzania katika maadili mazuri kwa kutoa nasaha mbalimbali kila siku ya ijumaa usiku kuanzia saa 3:00-4:00  kwa kuituma Redio ya Arusha one  fm(101.6 )

CHANGAMOTO
Ndugu mgeni rasmi palipo na mafanikio hapakosi changamoto , umoja huu unachangamoto zifuatazo:-
1-Ukosefu wa fedha kwa ajili ya survey pamoja na uwekaji wa lizi katika ardhi iliyo nunuliwa.
2-Ukosefu wa fedha kwa ajili ya michoro(ramani).
3-Ukosefu wa fedha kwa ajili ya usajili wa umoja, ambapo kadirio la chini  ilikuyafanikisha hayo ni shilingi milioni tano.
4-Ukosefu wa wahisani kwa ajili ya shughuli ndogondogo za umoja kama usafiri n.k
Mwisho:
Tunakushukuru kwa kuungana nasi katika hafla hii natunakuombea M.Mungu akurudishe salama nyumbani kwako na tunakutakia majukumu mema ya ujenzi wa taifa  Aamin.

0 comments:

Post a Comment

Copyright @ 2014 UWASUWA.

Designed by Japhary | Japhary Juma