Kongamano la Miiraji Tarehe 25/05/2014 saa 2:00 asubuhi Ukumbi wa CCM Mkoa - Arusha. More... Click Here!


Monday, 30 June 2014

MUFTI SHEIKH ISSA BIN SHABA SIMBA ATUA ARUSHA

Mnamo majira ya saa 8:30 mchana makhasimu wawili  { BAKWATA  "A" na  BAKWATA "B" } walikutana kwa ajili ya kumpokea mufti wa Tanzania Sheikh Issa Shaban Simba katika kiwanja cha ndege cha kisongo ambapo BAKWATA A wakiwa wanaongozwa na Sheikh wa mkoa Sheikh Shaban Juma wakati BAKWATA B wakiwa wanaongozwa na Imamu Mustafa Kihago,BAKWATA A walitangulia kufika kiwanjani hapo, Sheikh wa Mkoa akiwa anaendeshwa na dreva wake  mwnyekiti wa BAKWATA Mkoa bwana Muhammad Marawi wakati  BAKWATA B dreva wake akiwa ni bw.Abdul aziz Mkindi wote kwa pamoja waliingia ndani na kumlaki mgeni wao mheshimiwa Muft huku bwana mstafa akijitahidi kuchukuwa kumbukumbu kwa kupiga picha kila tukio ,na hatimae wote walitoka nje ya uwanja wa ndege na kila kundi kuingia kwenye usafiri wake  na kuungana pamoja katika masafara ulio kuwa ikiongozwa na Trafiki mwenye pikipiki na kushika barabara kuu itokayo Singida kuelekea Arusha mjini kwa kukatia kona ya Nairobi na kuishia Hoteli ya Naura spring ilyopo maeneo ya sanawari ambapo ndipo alipo fikia mheshimiwa mufti na wenzake kwa ajili ya kupumzika ili kesho tarehe 1/7/2014 sawa na ramdhan 3/1435 kuweza kuongea na waislamu wa jiji la Arusha katika msikiti mkuu wa ijumaa. Endelea kufuatilia habari hizi muhimu kama tutakavyo kuletea kesho inshaalla.....

Sunday, 29 June 2014

WAISLAMU WA JIJI LA ARUSHA KESHO SIKU YA JUMA TATU 30/6/2014 WATARAJIA KUMPOKEA MUFTI WA TANZANIA

mheshimiwa mufti aelekea jijini Arusha
Ziyara hiyo imethibitishwa na Sheikh wa Mkoa huo Sheikh Shaban bin Juma kwa kuwataka waislamu wote weye kuwa na fursa wajitokeze kwa wingi kwenye mapokezi hayo yatakayo anza baada ya swala ya adhuhuri  kuelekea kiwanja cha ndege cha kisongo kwa ajili ya mapokezi kama tukavyo kuwasilishia habari kamili hiyo kesho endelea kufuatilia habari hizi yawezekana ukapata jambo.....

Saturday, 28 June 2014

MIANZINI LEO HAPAKUTOSHA




Katika viwanja vya madrasa hii leo  ausbuhi walikuwa wakiadhimisha mwaka wa 14 tangu kuanzishwa kwake  rasmi  mwaka  2000 .Madrsa hii ilianza na wanafunzi watano(5) wakati huo wakisomea katika nyumba ya Baisaid mke wa marehemu saidi migire ,pia tunatoa shukurani nyingi kwa mama huyo kwahivi  sasa ametujengea madrasa kitu ambacho inatakiwa iwe ni mfano wa kuigwa kwa waislamu wengine, madras hii maendeleo yak e ni mazuri kwani hivi sasa ina wanafunzi mia mbili(200) na kama ilivyo kawaida yake kabla ya kufunga madarasa hufanywa maadhimisho ya kielimu ambapo wanafunzi  huwa wakaonyesha vipaji vyao mbalimbali  kwa kufanya maonyesho ya kielimu na yote hayo ni kwa juhudi za maustadh wake ambao ni  UstadhMohamed Ally na Ustadh Dhulkifli  Shaban Madrasa hii inasomesha masomo mbalimbali kamavile Qur-an,Hadith za mtume Sira n.k. Maonyesho hayo yalianza asubuhi na kumalizika jioni na mwisho wa maadhimisho ustadh alitoa shukrani nyingi kwa wote walio fanikisha madhimisho hayo

Friday, 27 June 2014

KHUTUBA ZA MISIKITI MINGI ARUSHA ZAHIMIZA WAISLAMU KUFUATILIA MWEZI MUANDAMO KWA KUUTAZA KWA MACHO

Hayo yameelezwa leo hii wakti wa swala ya ijumaa ili kuwaepusha waislamu na poropoganda za redio imani ambayo ikifikia tarehe hizi inakawaida ya kusema uwongo ili kuwahadaa waislamu waweze kufunga na kufungua kwa matashi yao kwani mwaka juzi walitumia lugha ya ulaghai kwa kusema kwamba"Mwezi umeonekana maeneo ya kondoa  na mwaka ulifuata walidai kuwa mweezi umeonekana mwanza na kuwahadaa waislamu kwa kumuapisha mwanamke mmoja eti ameuona mwezi yeye na watoto wake watatu,Pia mwaka jana wakiendelea na ulaghai wao kwakusema  kuwa mwezi umeonakana kibiti lindi na ameuona mwalimu wa shule na wanafunzi wake",maneno ambayo sikweli kwani UWASUWA walijitahidi kuwasiliamna na waislamu wa sehemu hizo nawaislamu hao kusema kuwa maeneo yao mwezi haujaonekana Maimamu ambao wako katika UWASUWA wamejitahihidi kuwafahamisha waumini wao kutokana na hali ya mambo yanavyo kwenda ili wasije wakaingia katika mkumbo wa kufunga na kufungua pasi na kuona mwezi kitu ambacho kiislaamu ni kosa kubwa na  hasa katika zama tulizo nazo.

Sunday, 15 June 2014

SHUGHULI ZA MADRSASA ISTQAMA ZA PAMABA MOTOTO

Maadhimisho yanayoendelea katika misimu hii ya kufunga Madrasa mbalimbali kwa ajili ya kuukaribisha Mwezi mtukufu wa Ramadhani, madrasa ya Istiqamah Fidifosi pia haikubakia nyuma ktk hilo .Asubuhi ya leo 15/6/2014 wameanza Maadhimisho yao  kwa ufunguzi wa Qur-an iliyosomwa na ustadh Issa Khamis na baada ya Qur-an ilombwa dua na imamu wa msikiti wa fidifosi Sheihk Mwinyi Kambi na kfutiwa na kiburudisho cha Qaswida iliyoimbwa na Madarasa ya Izzaddin Urundini chini ya usimamizi wa Mwl.Swalehe Abdallah .Baada ya kiburudisho hicho cha qaswida Awamu ya kwanza ya shughuli hiyo ilianza kwa mashindano ya qur-an ya kundi la kwanza la juzuu mbili yaliyo shirikisha washiriki tisa na kufuatiwa na kundi la pili la juzuu tatu lililiko shirikisha washiri watano na baada ya mashindanano hayo  hivi sasa yanaendelea maonyesho kama tutakavyo kuletea habari kamili pamoja na picha  baada muda kidogo

Friday, 13 June 2014

KONGAMANO LA TOFAUTI ZA MUANDAMO WA MWEZI LILILO ANDALIWA NA UWASUWA -28/SHABAN/1433

                                                                   SEHEMU YA KWANZA

ARUSHA WAISLAMU WASWEKWA NDANI

waislamu Arusha wamejikuta katika hali ngumu baada ya kukaidi hukumu ya mahakama iliyotolewa jana tarehe 12/6/2014 na kuwapa ushindi waislamu wa ahlus-suna waljamaa (BAKWATA)kuendelea kuutumia msikiti wa kuba
          Baada ya kutoka mahakamani waislamu  walielekea moja kwa moja na kuvunja kufuli ambazo zilikuwa zimefungwa wakati wa kusubiri hukumu ya mahakama.
Jafary Lema na kundi lake imeonekana kuwa ni chanzo cha vurugu katika msikiti huo,msikiti wa kuba umefungwa tena kwa muda
        tunaendelea kufuatilia habari hizi na tatakujuza kwa undani mambo yanavyo endelea kuwa karibu na blog hii

KONGAMANO LILILO TARAJIWA KUFANYIKA TAREHE 15/6/2014 LIMEHAIRISHWA MPAKA MWEZI WA NANE

LILE KONGAMANO LILILO TANGAZWA KUPITIA BLOG HII LIMEHAIRISHWA MPAKA MWEZI WA NANE tafadhali mfahamishe kila muislaamu mabadiliko hayo .

Wednesday, 11 June 2014

SHEIKH KISUA ALLY AKIWASILISHA MADA YA ISRAA KATIKA KONGAMANO LILILOANDALIWA NA UMOJA WA WALIMU

UNAWEZA KUISIKILIZA VIDEO HII KWA KUBOFYA HAPA

Tuesday, 10 June 2014

wanafunzi wa madrasa ya ahlubayt mtaa wa sakina ikiwa chini ya ustadh suleyman ramadhan

MAONYESHO YALIFANYIKA TAREHE  8/6/2014

Monday, 9 June 2014

MADRSAT SHAMSIYYATIL MAAROOF-MBUGA YA CHUMVI KWAMOROMB-ARUSHA

SIKU YA MAADHIMISHO YA SAFARI YA ISRAA NA MIIRAJ

MADRASAT SHAMSIL MAARIF


Sunday, 8 June 2014

HUYU NDIE USTADH SULEYMAN RAMADHAN WA MADRASA YA AHLUBAYT

AKITOA NASAHA KUHUSIANA NA MAHAFAL YA MWISHO WA MWAKA

MADRASA HII KWA HIVI SASA TUNASOMEA KWA BIBI AMINA

UATADHI SULEYMAN RAMADHANA AKIWA AMESIMAMA  NYUMA WA WANAFUNZI NA ALIYE KAA UPANDE WA KULIA NI USTADH MIRAJI KHAMIS NA ALIYEKAA UPANDE WA KULIA NI USTADH MASOUD
haya ni maadimisho ya mwaka wa tano tangu kuanza rasmi madrasa hii ya ahlubayt hapa sakuna

MADRASA YA AHLUBAYT MTAA WA SAKINA LEO 8/6/2014 WAKIWA KATIKA MAAFALI YA MWAKA WA TAMO

MWALIMU NA BAADHI YA WANAFUNZI NA WAZAZI KATIKA PICHA YA PAMOJA

Saturday, 7 June 2014

SIKU ILIYO ZINDULIWA BLOG YA UWASUWA

MHESHIMIWA KIBURWA  KIBAMBA AZINDUA BLOG YA UMOJA WA WALIMU WA AHLIS-SUNNA WAL JAMAA JIJINI  ARUSHA WALIO PEPEMBEZONI MWAKE NI MASHEIKH WA JIJI HILO.

Wednesday, 4 June 2014

QASWIDA YA MADRASAT RAHMAAN NJIRO

CHINI YA USIMAMIZI WA USTADHI TWAHA MOHAMED

Tuesday, 3 June 2014

MADRASAT SHAMSIL MAARIFIL ISLAAMIYYAH MKOA WA ARUSHA

Sehemu ya ndani ya madrasat shamsil maarif-mtaa wa shamsi(azimio)

WANAFUNZI WAKIKE WA MDRASAT SHAMSIL MAARIF -ARUSHA


MASJID ISTQAAMAH-ARUSHA

MSIKITI HUU BADO UKO KWENYE UJENZI-HII NI SEHEMU YA NYUMA YA MASJID ISTQAAMH

MADARASAT ISTQAAMAH KWA UPANDE WA NJE

WANAFUNZI WA KIUME WA MADRASAT ISTQAAMAH

MADARASAT ISTQAAMAH

DARASA LA KWANZA

MADRASAT ISTQAAMAH -ARUSHA

MWL.ABUBAKAR MAMBOLEO AKIWA NA BAADH YA WANAFUNZI WAKE DARASANI

MADRASAT ISTQAM-ARUSHA

BAADHI YA WANAFUNZI WAKIWA DARASANI

Monday, 2 June 2014

BAADHI YA WANAFUNZI WA MADRASAT RAHMAAN NJIRO-ARUSHA

MASJID TAWBA NJIRO & MADARASAT RAHMAAN

KWA USTADH TWAHA MOHAMED

Sunday, 1 June 2014

MAUSTADH WA MADRASAT SHAMSIYTIL MAAROOF KWAMOROMBO


BAADHI YA WANAFUNZI WA MADRASAT TAQWA WAKIWA DARASANI

USTADH KHALID MUSTAFA AKIFUNDISHA FANI YA HADIYTH

WANAFUNZI NA WALIMU WAO KATIKA PICHA YA PAMOJA

WALOSIMA MWISHO NI USTADHI MIRAJI AKIWA AMEVAA A NI KOTI JEUSI, USTADHI SWALEHE AKIWA KATI NA ANAEFUATA NI USTADH KHALID MUSTAFA

HII NDIYO MADRASAT TAQWA MAJENGO-ARUSHA

USTADHI MIIRAJI AKIWA NA BAADHI YA WANAFUNZI WAKE

VIONGOZI WA MADRASAT TAQWA WAKIWA NA WAGENI WAO KTK MAADHIMISHO HAYO

Add caption

Copyright @ 2014 UWASUWA.

Designed by Japhary | Japhary Juma