Kongamano la Miiraji Tarehe 25/05/2014 saa 2:00 asubuhi Ukumbi wa CCM Mkoa - Arusha. More... Click Here!


Saturday, 27 September 2014

MAULIDI MAKUBWA PAMOJA NA MAONYESHO YA KIILIMU YANAENDELEA HIVI SASA KATIKA WILAYA YA MONDULI

Leo hii kuanzia asubuhi mpaka usiku ni siku ya furaha kwa wakazi wa Monduli miji ya jirani, Madrasat salamatil Islaamiyyah chini ya Zawiyatil  Qadiriyatil Jailaniya kama ilivyo ada yake kila mwaka wakiadhimaisha mazazi ya Mtume Muhammad (s.a.w) ratiba ya shughuli yao inaonyesha kuwa sasa hivi ni maonyesho ya wanafunzi na baada ya maonyesho hayo itakuwa ni zaffa na baada ya swala ya isha mubashratan watamuadhimisha kipenzi chetu Sayyidina Muhammad(s.a.w) endelea kufuatilia blog hii tutakuletea habari kamili hivi punde

Wednesday, 24 September 2014

Sayyid Hassan Nasrulllah aweka wazi kuwa Marekani ni chanzo kikuu cha ugaidi Duniani

Katibu Mkuu wa chama cha Hizbullah cha Lebanon amesema kuwa Marekani haina ustahiki wa kiakhlaqi wa kuendesha mapambano dhidi ya ugaidi. Sayyid Hassan Nasrullah ameyasema hayo kupitia hotuba aliyoitoa jana usiku. Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon ameashiria juhudi zinazodaiwa kufanywa na Marekani kwa ajili ya kuasisi muungano dhidi ya Daesh na kusisitiza kwamba Hizbullah inalipinga kundi la Daesh na mirengo yote ya kitakfiri na yenye kushupalia vita na kwamba harakati hiyo inapambana na makundi hayo. Amesema kuwa harakati ya Hizbullah ya Lebanon iko tayari kuendesha mapambano dhidi ya makundi ambayo yanaua wananchi na kuwatishia raia na mataifa ya eneo hili. Sayyid Hassan Nasrullah aliongeza kama ninavyomnukuu" msimamo wetu kuhusiana na muungano wa kimataifa hauna uhusiano wowote na msimamo wetu kuhusiana na Daesh, kimsingi sisi tunapinga muungano wa kimataifa amma uwe dhidi ya Syria au dhidi ya Daesh au kinyume chake; na msimamo wetu haubadiliki kuhusiana na suala hilo na hatutakubali Lebanon iwe sehemu ya muungano huo wa kimataifa". Mwisho wa kunukuu. Nasrulllah amekumbusha kuwa Marekani ni chanzo kikuu cha ugaidi na muungaji mkono wa suala hilo na muungaji mkono pia wa utawala wa Kizayuni wa Israel. Amesema Marekani ilikuwa na nafasi kuu katika kuasisiwa makundi ya kigaidi na haina ustahiki wa kiakhlaqi wa kuendesha mapambano dhidi ya ugaidi. Katibu Mkuu wa chama cha Hizbullah cha Lebanon amesisitiza kuwa, kama alivyosema mara kadhaa Rais wa Marekani Barack Obama kwamba muungano huo ni kwa ajili ya kulinda maslahi ya Marekani, hivyo wao hawana maslahi yoyote na muungano huo.

Copyright @ 2014 UWASUWA.

Designed by Japhary | Japhary Juma