Katibu Mkuu wa chama cha Hizbullah
cha Lebanon amesema kuwa Marekani haina ustahiki wa kiakhlaqi wa
kuendesha mapambano dhidi ya ugaidi. Sayyid Hassan Nasrullah ameyasema
hayo kupitia hotuba aliyoitoa jana usiku. Katibu Mkuu wa Hizbullah ya
Lebanon ameashiria juhudi zinazodaiwa kufanywa na Marekani kwa ajili ya
kuasisi muungano dhidi ya Daesh na kusisitiza kwamba Hizbullah
inalipinga kundi la Daesh na mirengo yote ya kitakfiri na yenye
kushupalia vita na kwamba harakati hiyo inapambana na makundi hayo.
Amesema kuwa harakati ya Hizbullah ya Lebanon iko tayari kuendesha
mapambano dhidi ya makundi ambayo yanaua wananchi na kuwatishia raia na
mataifa ya eneo hili. Sayyid Hassan Nasrullah aliongeza kama
ninavyomnukuu" msimamo wetu kuhusiana na muungano wa kimataifa hauna
uhusiano wowote na msimamo wetu kuhusiana na Daesh, kimsingi sisi
tunapinga muungano wa kimataifa amma uwe dhidi ya Syria au dhidi ya
Daesh au kinyume chake; na msimamo wetu haubadiliki kuhusiana na suala
hilo na hatutakubali Lebanon iwe sehemu ya muungano huo wa kimataifa".
Mwisho wa kunukuu. Nasrulllah amekumbusha kuwa Marekani ni chanzo kikuu
cha ugaidi na muungaji mkono wa suala hilo na muungaji mkono pia wa
utawala wa Kizayuni wa Israel. Amesema Marekani ilikuwa na nafasi kuu
katika kuasisiwa makundi ya kigaidi na haina ustahiki wa kiakhlaqi wa
kuendesha mapambano dhidi ya ugaidi. Katibu Mkuu wa chama cha Hizbullah
cha Lebanon amesisitiza kuwa, kama alivyosema mara kadhaa Rais wa
Marekani Barack Obama kwamba muungano huo ni kwa ajili ya kulinda
maslahi ya Marekani, hivyo wao hawana maslahi yoyote na muungano huo.
Wednesday, 24 September 2014
Filled Under:
Sayyid Hassan Nasrulllah aweka wazi kuwa Marekani ni chanzo kikuu cha ugaidi Duniani
Posted By:
uwasuwa
on 01:30
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment