Walimu wa Madrasa baada yakuona maswali yamekuwa mengi kuhusu Maulidi ya Mtume Muhammad (s.aw.) kwamba inafaa kuadhimisha au haifai kuadhimisha, na badhi ya waumini kuuliza juu M.Mungu kwamba yuko wapi kwakutatizwa kwao na tafri ya juu juu ya inayo tolewa na baadhi yetu tafsiri ya sura iliyo teremshwa makkah sura ya 45 kuteremshwa sura yenye aya 135 matamko 1641 herufi 5242 kwa mpangilio wa msahafu ni sura ya 20 aya ya 5 yenye kujulikana kwa jina la surat twaahaa kama tunavyo iyona aya hiyo ( الرَّحْمَنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَى )
" Arrahmani, Mwingi wa Rehema, aliye tawala juu ya Kiti cha Enzi "Qur-an 20:5
Ili walazimu UWASUWA kutekeleza majukumu yao katika jamii ya kiislamu kwa kufanya muhadhara wenye mada kuu mbili mada ya maulidi na mada ya tawhidi ambapo mada ya maulidi ili wasilishwa na mwenyekiti wa UWASUWA ustsdh OMARY SAIDI JOUR kutoka Taasisi ya Hidaya Olmatejo na mada ya tawhidi iliwasilishwa na katibu idara ya Da'awa ustadh Hussein suleyman auf kutoka Taasisi ya Tarbiyatil ilsaam Jr
Mwenyekiti wa UWASUWA akiwasilisha mada yake kuhusu kufaa kumuadhimisha Mtume ( s.a.w ) mada ambayo nukuu zake nyingi ilikuwa ni kutoka kwa watu walio ishi na Mtume ( Maswahaba ) namana walivyo msifu Mtume ( s.a.w ) , na nukuu nyingine zikitoka kwa wanazuoni wakubwa wa kiislamu namna walivyo elezea kufaa kumsifu bwana Mtume unaweza pia kuzisikiliza mada hizo kupitia Chanel yetu ya youtube.Baadhi ya waumini wakiwa katika muhadhara huo wakipata faida mbalimbali juu ya kumsifu Mtume (s.a.w )
Ustadh Jabir Muhammad na Ustadh Miraj Khamis wakijaribu kurekodi mada kupitia simu zao za mkoni kama wanavyo onekana katika safuhii ya mbele.
Baada ya mada ya kwanza kukamililika MC wa Muhadhara huo Ustadh Athuman Hussein al marufu kwa jina la Msingidaa alimkaribisha mtoa mada wa pili Ustadh Auf kama tunavyo muona akiweka bidhaa zake mfukoni kwa ajili ya kusima ili kwasilisha mada yake inayo usiana na Tawhidi.
Katibu Idara ya Da'awa Ustadh Auf akiwasilisha mada yake akimuelezea M.Mungu yuko wapia jaribu kuchungulia kwenye youtube mwanzo mwisho naamini utapata vitu vizuri na imani yako itatulizana.
Nae Ustdh Khalid Mustfa kutoka Madrasat Taqwa Majengo ya juu akichukua kumbukumbu ili aweze kuwafikishia baadhi ya waumini ambao hakuweza kufika katika muhadhara huo kama alivyo nidokeza kutokana na unyeti wa mada zinazo endelea.
Nae Ustadh Omary kutoka Patandi ambae ni mukhitimu wa Maahadi ya kisauni Nchin Kenya aliye kaa kwa mshangao katika safu ya kwanza mbele baada ya kusikia namna mawahabi wanavyo potosha umma kwa kukataa kwao Majazi na Taawili ambapo Mtume ( s.a.w ) anamuombea Swahaba wake Abdallah Ibun Abbas Mwenyezi Mungu amfahamishe Ibn Abbas Tafsir na Taawili ya aya za Qur-an ambapo mtoa mada alipo alitoa mifano mingi mpaka kufikia kuielezea aya iliyoteremshwa Makka Sura ya 56 kuteremshwa sura yenye aya 182 matamko 860 herufi 3826 kwa mpangilo wa msahafu ni sura ya 37 aya ya 99 yenye kujilikana kwa jina la Surat Sswaaffaat M.Mungu anasema :-
وَقَالَ إِنِّي ذَاهِبٌ إِلَى رَبِّي سَيَهْدِينِ
na Mufasirina wana kubaliana kwamba hijra aliyo ifanya Nabii Ibrahima baada ya kutoka salama kwenye Moto alikwnda katika mji wa Shamu mtoa mada akasema "kwa mujibu wa mawahabi wanaokataa taawili na majazi wakichukuwa dhwahiri ya aya kwamba M.Mungu alikuwa yuko kwa maaan Nabii Ibrahimu alihamia mji wa shamu "
إِنَّا لِلّهِ وَإِنَّـا إِلَيْهِ رَاجِعونَ
Huu ni msiba mkubwa .
UWASUWA wanakuahidi mwezi ujao kukuletea Muhadhara mwingine Mkubwa kushinda huu mada kuu itakuwa ni Funga ya Ramadhan je,twatakiwa kufunga kwa kufuata mwezi utakapo onekanapopote Duniani au kila watu wa mji wanakuona kwao.
Kwa sababu kuna Redio moja hapa Nchini wanasema ni yakiislamu ikikaribia muandamo wa mwezi wa Ramadhan ina amua kusema uongo mwaka majuzi tulidanganywa kuna mwanamke Mkoa wa Mwanza yeye na familia yake tu wameuona mwezi na UWASUWA walipo jitahidi kuwasiliana na waislamu wa Mwanza waislamu wa Mwanza walikanusha habari hizo .
Na mwaka uliofuata tulidanganywa kuwa huko Kibiti Lindi Mwalimu wa shule na wanafunzi wake wameuona Mmwezi na tulipo lifutilia hilo kwa Masheikh wa maeneo hayo pamoja na Waumini wao walikanusha kwa nguvu zote taarifa hizo za uzushi kwa ajili ya maslahi fulani
UNAWEZA KUZIPATA BAADHI YA TAARIFA ZETU KUPITIA KWENYE FACEBOOK AU YOUTUBE AU MOJA KWA MOJA KUPITIA BLOG HII .
0 comments:
Post a Comment