Kongamano la Miiraji Tarehe 25/05/2014 saa 2:00 asubuhi Ukumbi wa CCM Mkoa - Arusha. More... Click Here!


Saturday, 19 November 2016

Filled Under:

KONGAMANO KUBWA LA KIDINI LAFANYIKA MKOA WA ARUSHA LEO 19/11/2016


BAADHI YA KINAMAMA WA KIISLAMU WAKIWA KWENYE KONGAMANO

 KONGAMANO HILI LILIFUNGULIWA KWA QUR-AN TUKUFU ILIYOSOMWA NA SHEIKH MUHAMMAD MAHAMUUDU ABDULFATAAH,
MUDIYRU WA AL-AZHARI SHARIF MKOA WA ARUSHA SHEIKH RAJABU ABDUL HAAD FILFAL AKITOA UFAFANUZI KUHUSU KONGAMANO HILO LILILO KUWA LINA MADA KUU NNE AMBAZO ZILIKUWA ZIKILENGA SUALA ZIMA LA AMANI NA UTULIVU KATIKA JAMII

SHEIKH MKUU WA MKOA WA MANYARA SHEIKH MUHAMMAD KADIDI AKIWASILISHA MADA INAYO HUSU KUTOKUMWAGA DAMU ZISIZO NA HATIA NA ADHABU ATAKAYO PATA MWENYE KUZIPUUZA DAMU  HIZO AKINUKUU AYA KATIKA QUR-AN SURA 5 AYA 32 (MAIDAH)
"Kwa sababu ya hayo tuliwaandikia Wana wa Israili ya kwamba aliye muuwa mtu bila ya yeye kuuwa, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewauwa watu wote. "
NAE MGENI RASMI MHESHIMIWA IDDI HASSAN IDDI KIMANTA MKUU WA WILAYA YA MONDULI AKIMUWAKILISHA MKUU WA MKOAA WA ARUSHA ALIANZA KWA KUPONGEZA SANA KONGAMANO HILO NA KUSISITIZA KUENDELEZA SEMINA NA MAKONGAMANO KAMA HAYO YAFANYIKE MARA KWA MARA KATIKA MAENEO MBALIMBALI YA NCHI YETU

PIA SHEIKH WA WILAYA YA MONDULI SHEIKH MWINSHEE SALIMU NAE HAKUBAKI NYUMA KATIKA KUSISITIZA AMANI YA NCHI, NA KUKEMEA VIKALI KITENDO CHA BAADHI YA WATU KUJICHUKULIA MADARAKA NA MAJUKUMU YASIYO WAHUSU KWANI KUFANYA HIVYO NDIO CHANZO CHA VURUGU NA UVUNJIFU WA AMANI SEHEMU HUSIKA.
SHEUKH RAJABU KIUNGIZA AKIWA NA SHEIKH WA MKOA WA MANYARA WAKIFUATILIA KWA KARIBU KONGAMNO HILO



MUDIYRU WA MARKAZI YA CHANG`OMBE JIJINI DAR ES-SALAAM SHEIKH AWADHI ABDUL-ADHIYMU AKIKABIDHI ZAWADI YA MKUU WA MKOA KWA MKUU WA WILAYA YA MONDULI 

 MKUU WA WILAYA AKITOA SHUKURANI ZA DHATI KWA KUPOKEA ZAWADI KWA NIABA YA MKUU WA MKOA Mh.Mrisho  Gambo
HAWA NI BAADHI YA WAUMINI WAKIWA KWENYE KONGAMANO HILO
MASHEIKH WAKITATHMINI NAMNA KONGAMANO LILIVYO FANA






0 comments:

Post a Comment

Copyright @ 2014 UWASUWA.

Designed by Japhary | Japhary Juma