Kongamano la Miiraji Tarehe 25/05/2014 saa 2:00 asubuhi Ukumbi wa CCM Mkoa - Arusha. More... Click Here!


Saturday, 24 June 2017

Filled Under:

HIVI NDIYO YALIVYO KUWA MASHINDANO YA KUHIFADHI QUR-AN 29/RAMADHA/1438 SAWA NA 24/6/2017

Katika Mashindano hayo yaliyo shirikisha Madrasa nane ( 8 ) za Jijini Arusha mbazo ni Hidaya kutoka Olmatejo,Darul Qur-an kutoka Sombetini, Nuri kutoka Ngarenaro ,Manazilul Abraar kutoka kwa morombo, Arusha Islamic Center kutoka Majengo ,Abdurahmaan Bin Auf kutoka Olmatejo , Swafa kutoka Kaloleleni na wenywji wao  Shamsili Maarif kutoka Shamsi.
KIJANA ABDULHAKIMU MUHAMMAD ALIYE VAA KOFIA NYEUPE NDIYE ALIYE SHIKA NAFASI YA KWANZA KWENYE KUNDI HILI LA JUZUU MOJA NAKUZADIWA SH 50,000/=  ,ANAYE FUATA KATIKATI MTOTO AMANI AYOUB SHIJA ALIIBUKA KUWA MSHINDI WA PILI  NA ALIZADIWA SH 30,000/=NA KIJANA ABDULRAHIMU JUMA (ALOLOO) ALIBUKA KUWA MSHINDI WA TATU NA ALIZAWADIWA SH 20,000/=
Baadhi ya walio hudhuria katika mshindano hayo kama tunavyo waona na miongoni mwao ndio mara ya kwanza kushiriki mashindano ya qur-an hapo anaonekana mwanafunzi Amani Ayoub shija ( mshindi wa pili wa juzuu moja) akiwa ameinamisha kichwa chini akifiria hivi anaweza kufanya vizuri pia ukimtazama mwanafunzi Abdurahimu Juma Aloloo ( mshindi wa tatu wa juzuu moja )  akiwa ameshika mashavu huku akitafakari mchuano namana ulivyo kuwa mkali
Mzee Ally Kassu baada ya kustaafu mashindano ya kuendesha magari ameibukia kwenye mashindano ya kuhifdhi Qur-an na hapo akichukuwa zawadi baada ya kufanya vizuri katika mashindano hayo
Majaji wa masindanano hayo wakijumuisha max baada ya makundi yote manne kusoma aliyeshika kalamu ni Ustadhi Hussein Hassan Myuyi ambae ni katibu wa Umoja wa Walimu Mkoa Arusha anaefuata  ni Ustdhi Gingi anajumuisha max ambaye  ni mmoja miongoni mwa walimu wa kituo maarufu cha kuhifadhisha Quran Jijini hapa kituo cha abdurahmaan bini auf cha hapo olmatejo na anayefuata ni sheikh Hadiyyu Hussein Lukarange ambe yeye ni Naibu Mudiyr wa Markazi ya Azhar Sharif ya Jijini Arusha
kijana mwenye kanzu na kofia nyeupe (Thabiti Salimini) kutoka Shamsil Maarif aliibuka kuwa mshindi wa kwanza wa juzuu tatu na alizawadiwa sh 80,000/= na anae fuata mwenye kilemba chekundu kijana Saadat Abdullahi kitoka Taasisi ya Hidaya Olmatejo alikuwa mshindi wa pili wa juzuu tatu na alizawadiwa sh 50,000/=  na Bw.Mahmudu Sufiyan muendesha bodaboda maarufu wa kijiwe cha Shamsi aliweza kuipokonya nafasi ya tatu na alizawadiwa sh 30,000/=  katika mashindano ambayo yalikuwa na mchuano mkali  katika kundi hilo lililo shirikisha washiriki ishirini na moja (21)

kijana mdogo katikati ( Luqman mohamed ) kutoka kituo cha Abdirahmaan bin Auf  olmatejo Alijinyakulia nafasi ya kwanza na kuzawadiwa sh 100,000/= ,anaye fuatia  Kijana Hambali Hambali Mohamed aliye vaa kofia  kutoka Arusha Islamic Center alichuwa nafasi ya pili na kuzawadiwa sh 80,000/=  na kijana Issa Mohamed kutoka Madrasat Nuri Ngarenaro aliye vaa kilemba kichwani  alishika nafasi ya tatu na kuzawadiwa sh 50,000/=

Mshindi wetu wa kwanza katika kundi hili la juzuu tisa ( 9 ) alikuwa   ni Hamza bin Ally kutoka kituo cha tahfidhul Quran cha Abdurahman bin Auf hapo olmatejo na alizawadiwa sh 150,000/= nafasi ya pili ilichukuliwan na  Binti mdogo aliye vaa hijabu nyeusi ( Hajra bint Rashidi ) kutoka Darul Qur-an sombetini  alizawadiwa sh 100,000/=na nafasi ya tatu ilchukuliwa na Swaumu bint Issa Khamis kutoka shamsil maarif  alye vaa jilbabu rangi ya maziwa na ufito wa rangi ya kijani  naye alizawadiwa sh 80,000/=
Ustadhi Masoud Hussein Salimu aliye shika  microphone ambaye ndiye mratibu mkuu wa mashindano hayo kabla ya ugawaji wa zawadi alielezea kiufupi namna ambayo mashindano yao yanavyozidi kukuwa makubwa mwaka hadi mwaka na kutoa mwito kwa wahisani mbalimbali waweze kujitokeza kudhamini mashindano hayo ,
Naye naibu Mwenyekiti wa Umoja wa walimu Mkoani Arusha Sheikh Juma Haji Mtandaya wapili kutoka upande wa kulia alitoa msisitizo wa kuwa na mchujo kabla ya kufanya mashindano ya Qur-an kwani wako baadhi ya wanafunzi wanaingia kwenye mashindano ili hali ni wabovu hawana vigezo naakatolea mfano wenzetu Dar-es-salaam wao wanafanya mchujo mpaka mara tano hivyo basi anawaomba wanaoandaa mashindano haya ( shamsil maarif  ) mwakani watakapo andaa tena mashindano  wawafanyie mchujo kabla ya kuingia katika mashindano .
             Khalifa Abubakar Saidi aliye shika kichwa akimuwakilisha Sheikh Salimu Mubarack (Sayyid Sujjada ) ndiye alikuwa mgawaji zawadi kwa niaba ya sheikh kwa washindi na washiriki wa mashindano hayo


0 comments:

Post a Comment

Copyright @ 2014 UWASUWA.

Designed by Japhary | Japhary Juma