PIGO KUBWA WAMELIPATA WALIMU WA DINI PAMOJA NA WAISLAMU WA JIJI LA ARUSHA KWA KUONDOKEWA NA KIPENZI CHAO USTADH HUSSEIN
إِنَّا لِلّهِ وَإِنَّـا إِلَيْهِ رَاجِعون |
Al-maruhumu Ustadhi Hussein Hassan Rashid Myuyi (1977-2018) marehemu Hussein Hassan alizaliwa mwaka 1977 hapa mkoani Arusha ,maremu Hussein yeye amezaliwa kutoka katika familiya ya Mzee Hassan Rashidi na bi:Shamiymu binti Maulidi hapo mtaa wa makaburi ya baniyani, marehemu Hussein ni kijana wa pili kuzaliwa katika familiya ya mzee Hassan akiwa ametanguliwa na dada yake mkubwa aitwae Leyla bint Hassan,watatu akiwa ni mdogo wake aitwae Twaha bin Hassan,wanne akiwa ni Iliyasa bin Hassan na akifuatiwa na kitinda mimba wao aitwae Zamzam bint Hassan hawa watano wote ni watu wa tumbo moja katika familia ya mzee Hassan lakini kabla ya wao kuzaliwa wanao wakubwa zao watatu ambao wamechangia mama ambao ni bwana Yunusi Ally Yusufu Ally na Fatuma binti Ally Mkungu .
Marehemu Ustadh Hussein alianza harakati za kusoma dini akiwa na umri wa miaka sita yaani 1986 kama alivyo lielezea hilo Sheikh na Mwalimu wake wa kwanza Ustdhi Juma Salimu Tura nakulithibitisha hili ndugu yake na marehemu aitwae Iliyasa
MWALIMU WAKWANZA WA MAREHEMU USTADHI HUSSEIN HASSAN AKIWA NYUMBANI KWAKE HAPO MTAA WA SHAMSI JIRANI NA MAKAO MAKUU YA UWASUWA JIJINI ARUSHA |
Sheikh Juma anasema nilimpokea Ustdhi Hussein akiwa na
umri wa miaka sita wakati huo Madrasa yetu ikiwa mtaa wa makaburi ya baniyani
kwa Mzee Kisiju mwaka 1983 ambapo kundi lake likiwa ni la pili likiwa
limetanguliwa na kundi la kwanza la kina Issa Cheupe.mwalimu Husssein alianza
kusoma shule ya msingi mwaka 1986 katika Shule ya msingi Ngarenaro na kumaliza
mwaka 1993.
Marehemu Hussein alilelewa na wazazi wake katika maadili ya Dini
pamoja nakuwa alikuwa anasoma shule wakati huo huo alipenda kusoma madrasa kitu ambacho kwa baadhi ya watoto hakipo pia baadhi ya wazazi hawana kwa kisingizio cha kwamba mtoto hawezi kusoma shule na madrasa kwa pamoja,baada tu ya kumaliza shule ya msingi alidumu katika
madrasat Nuuri mpaka pale Sheikh Abdulkadir Sufi alipo asisi madrasa yake mtaa
wa shamsi, madrasa ambayo ilikuwa ikisimamiwa na walimu wawili (Sheikh Shaban
bin Jumaa ambaye kwasasa ni Sheikh wa Mkoa wa Arusha na mwenzake Sheikh Simba M.Khalfan) ndipo marehemu Hussein alihamia kwa muda na kwenda kusoma Madrsa hiyo ya shamsi na badae alirudi
kuja kuendelea kusoma hapa madrsat nuuri wakati huo mwalimu Hussein nikijana "ndipo
nilipo waita baadhi ya wazazi yaani Marehemu Mzee Hassan baba yake na marehemu Ustadh Hussein amabaye aliishafariki toka mwaka 2001,Mzee Juma Ndao,Mzee Hussein Mori na Mzee Hussein Mfipa .
Baada ya
wazee hao kufika nikawapa fikra yangu kuwa hawa watoto wetu tuwatoe waende
wakaongeze elimu tuwapeleke kusoma nje ya Arusha wakati huo Sheikh Abdallah Swalehe Suna akifundisha Madrasa ya Riyadhwa hapo kona ya Nairobi na Sheikh Sharifu akifundisha madrasa yake hapo msikitini ngarenaro katika msikiti mdogo
waliafiki fikra yangu ndipo nikawaambia subirini kwanza nimfikishie Sheikh Siraji,baada ya kumfikishia Sheikh Siraji bin Salimu Nymbwa alikubali fikra
hiyo na kuwaita wazee hao baada ya kuongea nao nakufikia muwafaka ndipo Sheikh Siraji M.Mungu amrehemu alianza michakato ya safari na baada ya kukamilika
aliwapeleka Mambrui huko lamu Nchini Kenya kwa Sheikh Sharif Sayyid Muhammad Albedhi." wakaanza kusoma huko na badae walihamia Madrsat Najah kwa Sheikh Sharif Mwinyibaba huko waliendelea na masomo yao mpaka walipo maliza wakarudi
kwa Sayyid Muhammad Albedhi kwa ajili ya kutaka baraka zaidi za Sheikh yaani walipo anzia kusoma baada ya kutoka Tanzania lakini wakati huo mwanafunzi mwenzao Saidi Hussein alikuwa
ameisha katisha masomo yake waliobaki ni Mzamilu Juma Ndao,Hajji Hussein Mfipa,Twaha(Salimu)Salimu Juma Tura na marehemu Ustadh Hussein Hassan.
Baada ya
kukamilisha masomo yao waliruhusiwa kila mmoja arudi aliko toka ili akaendeleze
kazi ya Dini.marehemu Ustadhi Hussein kabla ya kurudi rasmi aliamua kuongeza
miaka mitatu (3) na baada kuikamilisha alirudi nyumbani kwa ajili ya
kufanya kazi ya M.Mungu,
Tulimpokea kwa furaha na kuwa nae hapa Madrasat Nuuri baada ya muda kupita Mwalimu Hussein aliomba ruhusa kuwa amepata nafasi ya
kusomehsa Nairobi nchini Kenya baada ya kunipa taarifa hiyo nilimkatalia
asiende naye pasi na kinyongo alitii tukaendelea kuwa pamoja nae .
Baada ya Madrasa ya Sheikh Sharifu kusimama ndipo sisi tulihamia rasmi hapo msikitini na
wakati huo aliisha kuja Ustadh Juma Yahya wote tukawa tunfundisha Madrasat Nuuri na madrsa ikazidi kunawiri.
Iipo fika mwaka 2001 Mzee Hassan Rashid Myuyi baba ya marehemu ustadh hussein alifariki
na kipindi hicho kilikuwa kizito sana kwa familia ya Mzee Hssan lakini Ustadhi Hussein alijitahidi kuwafariji ndugu zake khususwani wadogo zake ambao walikuwa bado masomoni (Twaha na Iliyasa) kwani wao wakati huo walikuwa wanaendelea na masomo ya sekondari.
Marehemu Ustadhi Hussein ile desturi yake ya kupenda kusoma alikuwa bado anayo kwani ndoto yake ilikuwa katika elimu ya sekula pia japo afike chuo kikuu kwa hivyo baada ya kuwa amepata elimu ya dini kwa mara ya kwanza aliamua kujiunga na kozi ya Uwalimu katika Chuo cha Kirinjiko na baada ya kukamilisha kozi hiyo aliamua kuendelea kuifanyia kazi elimu aliyo ipata kwakuanza kufundisha
dini katika Markazi ya Wamisri ya Al-azhar Sharif ya Jijini Arusha wakati huo Mudiyr alikuwa ni Fadhwiylatu Sheikh Ally Mukhtaar M.Mungu amrehem
Mwalimu Hussein pamoja nakusomesha Madrsat Nuuri na Madrsat Azh-har bado alikuwa ni
mwenye kupupia mambo ya kheri kwani wakati huo pia alikuwa ameisha jiunga na
umoja wa walimu wa madrasa pia alikuwa kaimu katibu akiwa amekaimu nafasi ya
katibu wa kwanza wa UWASUWA Ustadhi Haruna Abdalla na badae alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu kutokana na utendaji wake mzuri kwa hakika alikuwa mchapa kazi hodari.
Pamoja nakuwa na majukumu mengi hakukata tamaa katika kujiendeleza alimua kujiunga na program za qualifying test(qt)ambapo alisoma na kufaulu vizuri katika mitihani ya kidato
cha nne na ulipo fika mwaka 2006 aliamua kuanza maisha mapya ya kuishi na mke
kwa kufunga ndoa ambayo iliyefungisha ndoa hiyo alikuwa ni Al-Alaama Sheikh Ally Mukhtaar .
Wiki
mbili kabla ya kufariki marehemu Ustadh Hussein alituhimiza wanauwasuwa kuwahamasisha walimu mbalimbali kuendelea kujiunga na umoja nakusisitiza kuwa umoja ni nguvu kama inavyoonekana chati aliyo iandaa ili twende nayo katika ziyara Wilayani Karatu.
Siku sita kabla ya kufariki marehemu Hussein (katibu wa uwasuwa) aliitisha
kikao cha dharura (19/2/2018) na Agenda ilikuwa ujennzi wa Msikiti wa kudumu wa Daarul Mustwafa kwa ufadhili kama ambavyo maandishi ya hati yake yanavyo onekana katika kikao ambacho
kilikuwa nawajumbe kumi na mbili
(Ustadh Omary Saidi,Hussein Hassan,Masoud Hussein,Athuman Hussein,Jabir Muhammad,Issa M.Kapama,Hussein Suleymaan Auf,Khalid Mustafa,Abubakar Mamboleo,Miraj Khamis katibu wa madrasa ya Darul Mustwafa na Mwalimu Yahya wa Madrsat Daarul Mustwafa).
HIKI NDICHO KILIKUWA KIKAO CHA MWISHO NA KATIBU WETU USTDHI HUSSEIN HASSAN MYUYI NA ILIKUWA NI ZAMU YA USTADHI ISSA KAPAMA KUCHANGIA MADA |
Jambo laajabu lililo dhihiri siku hiyo
wengi wa Walimu walijitahidi kupiga picha kitu ambacho si chakawaida kwenye
vikao ambavyo huwa vinafanyika mara kwa mara, kumbe picha hizo zilikuwa ndio picha za
mwisho tukiwa na katibu wetu Ustadh Hussein kama picha zinavyo onekana hapo chini.
Siku moja kabala ya kufariki
Namnukuu Ustadh Khalid Mustafa "Jana jioni mimi ,Mwenekiti na katibu wa UWASUWA tulikuwa kwa mwanasheria kwa ajili ya kukamilisha mkataba wa kumkabidhi muhisani kazi ya ujenzi wa msikiti kama kikao kilivyo tuagiza ili jumatatu tumkabidhi na kazi ianze ."
Marehemu Ustadhi Hussein amefariki siku ambayo idara ya da`awa
(kufikisha ujumbe k.v mawaidha au nasaha n.k )kupitia katibu wake Ustadhi Miraji alikuwa ameisha tutangazia kuwa baada ya swala ya magharibi tutakuwa na
ziyara ya Da`awa Masjidi Nabawiy Mtaa wa Uswahilini ungalimited kwa Sheikh Ayoub na ataye wasilisha mada atakuwa ni Ustadh Issa Muhammad Kapama kutoka fidifosi,
kama ilivyo kawaida ya
umoja huu kila siku ya jumapili baada ya swala ya maghrib huwa awakatembelea Misikiti mbalimbali ya Jiji la Arusha
marehemu Ustadh Hussein pia
alikuwa ameisha tia nia ya kwenda kwenye ziyara hiyo lakini saa chache kabla ya
kuingia maghrib alitutoka baada tu ya mwenyekiti wa umoja Sheikh Umar Saidi Jour kuthibitsha kifo chake alijitahidi kumpata
katibu wa Idarara ya Da`awa ili
asitishe ziyara na awafahamishe wanauwasuwa kuhusiana na msiba mzito ambao wameupata wana uwasuwa baada ya Idara kupata taarifa za msiba Idara ya Da`awa ililazimika kusitisha ziyara
hiyo.
Aama kuhusu kifo chake nikama alivyo simulia kifo hicho Ustadhi Athuman Hussein ambaye pia ni mwanauwasuwa namnukuu "leo saa 4 asubuhi tulialikwa hapo
sheli ya panoni kwa Mama Abdilahi kulikuwa na shughuli ya hakiki sote kwa
pamoja tukiwa na marehemu Ustadhi Hussein kwa ajili ya hiyo sunna ya hakiki shughuli ambayo imemalizika saa 6 ya
mchana baada ya hapo tulirudi haraka kwani tulikuwa na kikao kifupi cha harusi
ya kijana wetu wa madrasa (Issa Ramadhan) ambaye anatarajia kufunga ndoa yake
mwisho wa mwezi wa tatu 31/3/2018 baada ya hapo tulikwenda kwenye harusi ya Shafii Hamad Abdallah na bi Aziza Iddi hapa ngarenaro maeneo ya kibanda umiza
baada ya muda kidogo Sheikh Mahamud Salimu Nyambwa aliingia na kumuagiza Ustadh Hussein aijaze kabisa hiyo hati ya ndoa Ustadhi Hussein alianza kujaza
coppy ya kwanza na aliikamlisha alipoanza coppy ya pili alisema najisikia vibaya
mara tu tukaona anaishiwa nguvu tukaanza kumpepea gari ikasogea tukampeleka Hospitali
kwa babu Madakatari walimpokea na kuanza kumuhudumia mwisho wa yote walisema kuwa presha
ilikuwa imepanda sana na baada ya dakika chache akawa amefariki inna lilahi
waina ilaihi rajiun "
marehemu alikufa siku ya jumapili jioni na kuzikwa siku ya jumatatu katika makaburi ya fidifosi.
0 comments:
Post a Comment