Kongamano la Miiraji Tarehe 25/05/2014 saa 2:00 asubuhi Ukumbi wa CCM Mkoa - Arusha. More... Click Here!


Friday, 11 July 2014

Filled Under:

HOFU YA KWENDA KUSWALI WAISLAMU WA NCHINI MYANMAR YAENEA KWA KUOGOPA KUSHAMBULIWA NA MABUDHA

Waislamu wanaokandamizwa nchini Myanmar sasa wameshindwa kuenda kufanya ibada misikitini katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kutokana na hofu ya kushambuliwa na Mabudha wenye misimamo mikali. Imearifiwa kuwa Waislamu wa mji wa Mandalay ambao ni wa pili kwa ukubwa nchini Maynmar wanaogopa kuenda misikitini baada ya kushambuliwa wiki iliyopita na Mabudha wenye misimamo mikali. Maelfu ya Waislamu wa kabila la Rohingya wameuawa nchini Myanmar katika miaka ya hivi karibuni kufuatia hujuma za Mabudha wenye misimamo mikali nchini humo. Makumi ya maelfu ya Waislamu wamelazimika kuacha makazi yao nchini na kukimbilia kupata usalama katika nchi jirani,waislamu wa kabila Rohingya takriban ni asilimia 5% ya wakazi wote wa Nchini Myanmar {60,000,000}lakini pamoja na hayo wamekuwa wakikandamizwa,kudhulumiwa na kuteswa tokea nchi hiyo ipate uhuru wake mwaka 1948
      Umoja wa mataifa unasema waislamu wa kabila la Rohingya katika jimbo la Rakhine nchini Myanmar ni kati ya watu wanao dhulumiwa zaidi duniani

0 comments:

Post a Comment

Copyright @ 2014 UWASUWA.

Designed by Japhary | Japhary Juma