Zaidi ya Wapalestina 230 wameuawa shahidi katika
mashambulizi ya utawala haramu wa Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza. Idadi
hiyo imeongezeka baada ya uatawala huo kufanya mashambulizi mengine
dhidi ya makazi ya raia katika eneo la mashariki mwa eneo la Rafah la
kusini mwa ukanda huo. Raia watano waliuawa shahidi mapema leo katika
shambulizi jingine la ndege za kivita za utawala huo katika maeneo ya
Khan Yunus, Beit Lahya na Dirul-Balah huko Ghaza. Wakati huo huo
usitishwaji vita kwa masaa ulioitishwa na Umoja wa Mataifa kwa lengo la
kuwasilisha misaada ya kibinaadamu katika ukanda huo, umeanza
kutekelezwa. Kwengineko, duru za habari zinaeleza kuwa katika
mashambulizi ya siku 10 dhidi ya eneo la Ghaza, utawala haramu wa
Kizayuni umetumia tani elfu nne ya mada za miripuko katika eneo hilo.
Hayo yamebainishwa na mratibu wa harakati ya kuvunja mzingiro wa Ukanda
wa Ghaza, Bwana. Nabil Halak katika mahojiano aliyofanyiwa na kanali ya
habari ya Press TV na kuongeza kuwa, mashambulizi ya Israel dhidi ya
Ghaza ni mauaji ya halaiki yasiyo na mlingano. Aidha Nabil amebainisha
kuwa, asilimia 80 ya wahanga wa mashambulizi ya utawala huo katili ni
raia wasio na hatia, hususan watoto wadogo, wanawake na wazee.
Thursday, 17 July 2014
Filled Under:
HUKO GAZA KILA KUKICHA MAUWAJI YANAENDELEA NINI HATMA YA WAPALESINA
Posted By:
uwasuwa
on 13:56
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment