Mhadhiri na msomi mashuhuri nchini Marekani ndugu Arvam Noam Chomsky
amewakosoa
vikali viongozi wa Marekani kwa kutoa matamshi ya vitisho dhidi ya Iran.
Akihojiwa na Press TV mjini New York, Noam Chomsky amesema kuwa,
wanadiplomasia wa Magharibi na hasa Marekani wanatoa matamshi ya vitisho
dhidi ya Iran na hata wanathubutu kusema kwamba, chaguo la kutumia njia
za kijeshi bado liko mezani, katika hali ambayo utumiaji wa lugha za
vitisho dhidi ya nchi nyingine ni ukiukwaji wa sheria za kimataifa.
Msomi huyo mashuhuri nchini Marekani ameongeza kuwa, matamshi hayo ya
vitisho yanayotolewa na viongozi wa Marekani kuhusiana na miradi ya
nyuklia ya Iran yenye malengo ya amani yanaweza kutafsiriwa kwamba
Washington inaweza kutumia nguvu za kijeshi dhidi ya Iran. Marekani na
baadhi ya washirika wake wa Ulaya mara kadhaa wamekuwa wakiituhumu Iran
kwamba miradi yake ya nyuklia ina malengo ya kijeshi. Inafaa kuashiria
hapa kuwa, viongozi wa ngazi za juu wa Iran wamesisitiza mara kadhaa
kuwa, Iran kamwe haina mpango wa kutengeneza kombora la atomiki, kwani
mpango huo unakinzana na misingi ya sheria za dini tukufu ya Kiislamu.
Wednesday, 15 October 2014
Filled Under:
Vvitisho vya Marekani dhidi ya Mataifa mengine vyakosolewa
Posted By:
uwasuwa
on 21:53
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment