الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُم مُّصِيبَةٌ قَالُوا إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ
رَاجِعُونَ
Mshukiwa mkuu wa mashambulio ya kigaidi yaliyokuwa yakifanyika katika mji wa Arusha ameuawa baada ya kufyatuliwa risasi kadhaa na askari polisi baada ya kujaribu kuruka kwenye gari chini ya ulinzi mkali wa Polisi akisafirishwa kuelekea kwao kondoa kwa ajili ya kuonyesha mabomu mengine aliyo kuwa ameyaficha huko, Taarifa kutoka kwa kamnda wa Polisi Arusha ndugu Lebaratus Sabas zinasema kuwa, Yahya Omar Hassan Hela maarufu kwa jina la 'Yahya Sensei' ambaye inadai alikuwa mpangaji na mratibu wa mashambulio ya kigaidi mjini Arusha, ameuawa kwa kupigwa risasi wakati alipojaribu kuruka kwenye gari la polisi kwa lengo la kuwatoroka. Jeshi la Polisi limeeleza kuwa, mtuhumiwa huyo alikiri kuhusika na upangaji na uratibu wa mashambulio tisa ya kigaidi katika miji ya Arusha, Zanzibar, Mwanza na Dar es Salaam wakati alipohojiwa na jeshi hilo.
Miongoni mwa mashambulio yaliyofanywa na mtuhumiwa huyo ni lile lililofanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph lililopo Olasiti jijini Arusha, lililosababisha vifo vya watu watatu na majeruhi 36.
0 comments:
Post a Comment