Kongamano la Miiraji Tarehe 25/05/2014 saa 2:00 asubuhi Ukumbi wa CCM Mkoa - Arusha. More... Click Here!


Saturday, 11 October 2014

Filled Under:

KUNA NINI LEO KWA WANAFUNZI SEKONDARI YA URAKI NA LEKI TATU

Ni furaha zisizo elezeka kwa wanafunzi wa kiislamu wa shule hizo mbili walipo amua kuungana pamoja katika mahafali yaliyo fanyika Sekondari ya Uraki
SEHEMU KTK JUKWAA KUU LINAONEKANA LIMEPAMBWA NA BAADHI YA  WAGENI WAALIKWA






M.C MWALIMU ABUSHAKUR MUSTAFA ANA WAKARIBISHA WOTE WALIHUDHURI MAHAFALI HAYA KWA KUSEMA KUWA MGENI RASMI NDIO ANAINGI  HIVYO KILA ALIYE MBALI ASOGEE NA ACHUKUWE NAFASI YAKE KWA SABABU TUKO NJE YA WAKATI .FUNDI MITAMBO PIA HAKUCHEZA MBALI NA KAZI YAKE KAMA TUNAVYO MUONA



BAADA YA MC KUTOA TANGAZO LAKE KINABABA WALIWAHI NAFASI ZAO KAMA TUNAVYOONA

 
Kwa upande wa kina mama pia hawakubaki nyuma kwani wao ndio walionyesha kuwa na kiu zaidi katika mahafali haya ya mwaka wa nne.
      Baada ya kuwa watu wamekaa na kutulia mahafali yetu yalianzwa kwa dua ilombwa na mzee wetu mzee Amani kutoka masjidi majengo kufutiwa na Qur-an tukufu iliyo somwa na Amiri wa wanafunzi Leki tatu Ustadh Kisra Juma
        Ambpo mufasiri wa aya zilizo somwa alikuwa ni Sheikh Miraji Khamis  kutoka Masjid Taqwa
wa mjini Arusha ambapo alizama zaidi ktk aya hizi tatu zinazo sema:-
-                                                            إِنَّ لِلْمُتَّقِينَ مَفَازًا ﴿٣١﴾ حَدَائِقَ وَأَعْنَابًا ﴿٣٢﴾ وَكَوَاعِبَ أَتْرَابًا ﴿٣٣﴾     د 
       Na baada ya kutafiriwa aya hizo ilifutia mada ya kwanza ambayo iliwasilishwa na Imamu wa msikiti wa majengo mada ambayo ili beba mambo makuu mawili jambo lakwanza ilikuwa ni kuhusiana na Wazazi ,wazazi wanao wajibu wa kuzidi kuwasomesha watoto wao elimu zote Elimu ya Dinii kwa ajili ya akhera yao na elimu ya dunia kwa ajili ya duia yao na jambo la pili lili wahusu wanafunzi na zaidi sheikh alihimiza kuhusiana an adabu.
            Ambapo mada ya pili iliwasilishwa na Ustadh Masoud Hussein kutoka masjid Mahfuudh Mtaa wa shamsi mjni Arusha na na yeye alielezea uislamu namna  ulivyo himiza kuhusina na kutafuta elimu na alianza na aya ambazo zilisomwa na msomaji Qur-an wa pili katika mahafalia hayo Amir wa shule ya Uraki kijana Hamad Kundya aya ambazo zilikuwa ni zakwanza kushushwa katika Quran kwa mtume wetu muhammad ( s.a.w ) yaani katika surat alaq :-

اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ ﴿١﴾ خَلَقَ الْإِنسَانَ مِنْ عَلَقٍ ﴿٢﴾ اقْرَأْ وَرَبُّكَ الْأَكْرَمُ ﴿٣﴾ الَّذِي عَلَّمَ بِالْقَلَمِ ﴿٤﴾ عَلَّمَ الْإِنسَانَ مَا لَمْ يَعْلَمْ ﴿٥﴾
           Ambapo mada ya mwisho iliwasilishwa na sheikh Abdurahman Idrisa imamu wa masjid Irshad Ngarasero ambapo yeye alizama katika mashairi baada ya kuona mada ya kwanza ilizama ktk hadith na mada ya pili ktk Qur-an na zaidi aliamua kumuelezea msomi kwa kusema msomi ni mtu hatari sana endapo ataitumia elimu yake vibaya na upande wa pili msomi ni mtu mwenye manufaa sana endapo ataitumia elimu yake vizuri.
             Baada ya mada ya mwisho ilisomwa risala na mmoja ktk wahitimu wa kidato cha nne risala ambayo ilbeba ujumbe mzito unahusiana na taaluma ya kiislamu mashuleni ,upotevu wa maadili ya mavazi kwa wanafunzi wakike na uhaba wa nyenzo na hasa vitabu vya marifa ya uslamu ambpo seti moja ni shilingi elfu thelathini tu.
MGENI RASMI BWANA OMARY MSHANA KIBIDHIWA RISALA NA MSOMA RISALA NA BAADA YA RISALA UTOAJI VYETI ULIANZA KAMA TUNVYO ONA KTK TUKIO LINALO FUATA
MUHITIMU WA KIDATO CHA NNE BAADA YA ZAWADI

Baada ya ugawaji vyeti ulisomwa dua ya kufunga mahafali hayo na Mzee Amani mnamo majira ya asaa 1:15 watu wote walitakiwa waingie kwenye ukumbi wa chakula na baada ya hapo kila mmoja aliruhusiwa na hapo ndi mwisho wamahafali ya mwaka huu wa 2014










0 comments:

Post a Comment

Copyright @ 2014 UWASUWA.

Designed by Japhary | Japhary Juma