Kongamano la Miiraji Tarehe 25/05/2014 saa 2:00 asubuhi Ukumbi wa CCM Mkoa - Arusha. More... Click Here!


Thursday, 17 July 2014

HUKO GAZA KILA KUKICHA MAUWAJI YANAENDELEA NINI HATMA YA WAPALESINA

Wapalestina zaidi waendelea kuuawa huko Gaza
Zaidi ya Wapalestina 230 wameuawa shahidi katika mashambulizi ya utawala haramu wa Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza. Idadi hiyo imeongezeka baada ya uatawala huo kufanya mashambulizi mengine dhidi ya makazi ya raia katika eneo la mashariki mwa eneo la Rafah la kusini mwa ukanda huo. Raia watano waliuawa shahidi mapema leo katika shambulizi jingine la ndege za kivita za utawala huo katika maeneo ya Khan Yunus, Beit Lahya na Dirul-Balah huko Ghaza. Wakati huo huo usitishwaji vita kwa masaa ulioitishwa na Umoja wa Mataifa kwa lengo la kuwasilisha misaada ya kibinaadamu katika ukanda huo, umeanza kutekelezwa. Kwengineko, duru za habari zinaeleza kuwa katika mashambulizi ya siku 10 dhidi ya eneo la Ghaza, utawala haramu wa Kizayuni umetumia tani elfu nne ya mada za miripuko katika eneo hilo. Hayo yamebainishwa na mratibu wa harakati ya kuvunja mzingiro wa Ukanda wa Ghaza, Bwana. Nabil Halak katika mahojiano aliyofanyiwa na kanali ya habari ya Press TV na kuongeza kuwa, mashambulizi ya Israel dhidi ya Ghaza ni mauaji ya halaiki yasiyo na mlingano. Aidha Nabil amebainisha kuwa, asilimia 80 ya wahanga wa mashambulizi ya utawala huo katili ni raia wasio na hatia, hususan watoto wadogo, wanawake na wazee.

Saturday, 12 July 2014

MASHINADANO YA QUR-AN YANAYOENDELEA KATIKA VIWANJA VYA MADRASAT MUHAJIRINA NI KAMA IFUTAVYO

MC .WA MASHINDANO HAYO AKIWAKABIDHI MAJAJI MAJUKUMU YA KUSIMAMIA MASHINDANO HAYO
MWANAFUNZI WAILD SAID NA RADHWIYA AYOUB WAKISOMA QUR-AN KATIKA MASHINDANO HAYO
HILI NI JUKWAA LA KINA BABA WAKISIKILIZA QUR-AN KWA UMAKINI WA HALI YA JUU
MC AKIITIKIA DUA ILIYO SOMWA NA NAIBUL MUDIYR SHEIKH FADHIL


Baada ya kukamilisha kundi la kwanza  la juzuu moja tulielekea kuswali swala ya adhuhuri 


     Baada ya swala tulianza kama ifuatavyo kwanza tulisomewa Qur-an tukufu na sheikh mahmudu






KINA MAMA PIA HAWAKUBAKI NYUMA KATIKA MASHINDANO HAYO



MEZA KUU TUNAMUONA SHEIKH MUHAMMAD BAKAR AKIWA NA BAADHI YA MASHEIKH

MWENYEKITI WA CCM MKOA AKIWA WAMEFUATANA NA MWENYEKITI WA WILAYA WA BAKWATA SHEIKH HUSSEIN CHIFUPA
Endelea kufuatilia kwa karibu kupitia blog hii kuhusiana matokeo ya washindi kama tutakavyo kuletea kwa ukamilifu badae ........

Friday, 11 July 2014

HOFU YA KWENDA KUSWALI WAISLAMU WA NCHINI MYANMAR YAENEA KWA KUOGOPA KUSHAMBULIWA NA MABUDHA

Waislamu wanaokandamizwa nchini Myanmar sasa wameshindwa kuenda kufanya ibada misikitini katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kutokana na hofu ya kushambuliwa na Mabudha wenye misimamo mikali. Imearifiwa kuwa Waislamu wa mji wa Mandalay ambao ni wa pili kwa ukubwa nchini Maynmar wanaogopa kuenda misikitini baada ya kushambuliwa wiki iliyopita na Mabudha wenye misimamo mikali. Maelfu ya Waislamu wa kabila la Rohingya wameuawa nchini Myanmar katika miaka ya hivi karibuni kufuatia hujuma za Mabudha wenye misimamo mikali nchini humo. Makumi ya maelfu ya Waislamu wamelazimika kuacha makazi yao nchini na kukimbilia kupata usalama katika nchi jirani,waislamu wa kabila Rohingya takriban ni asilimia 5% ya wakazi wote wa Nchini Myanmar {60,000,000}lakini pamoja na hayo wamekuwa wakikandamizwa,kudhulumiwa na kuteswa tokea nchi hiyo ipate uhuru wake mwaka 1948
      Umoja wa mataifa unasema waislamu wa kabila la Rohingya katika jimbo la Rakhine nchini Myanmar ni kati ya watu wanao dhulumiwa zaidi duniani

KESHO TAREHE 12/7/2014 KUTAKUWA NA MASHINDANO YA KUHIFADHI QUR-AN YALIYO ANDALIWA NA MADRASAT MUHAJIRINA HIMO

tunatarajia kuwa na washiriki kutoka  mikoa ya Dar es saalm Arusha na  Kkilimanjaro karibu kwenye mashindano hayo kama tutakavuo kuletea habari kamili hiyo kesho endelea kufuatilia kwa karibu

Thursday, 10 July 2014

VIONGOZI WA DINI YA KIISLAMU JIJINI ARUSHA WASUSIA FUTARI ITAKAYO ANDALIWA NA MUNADHAMAT DAAWAT ISLAMIYA

Baada ya kung`amua hila wanazo penda kuzitumia wanataasisi hao wa munadhamat daawa ya jijini Dar-es-salaam  hasa hapa kwetu Arusha tumeamua kutohudhuria  semina ambayo inakusudiwa kufanywa kesho siku ya ijumaaa  tarehe 11/7/2014 kuanzia saa 8:00 mchana -saa12:00 jioni na kufuatiwa na futari, katika ukumbi wa ccm mkoa ambapo mualiko wao unasema  mgeni rasmi atakuwa mkurugenzi wa jiji la Arusha na mada itakayo wasilishwa itakuwa ni fursa za kiuchumi kwa waislamu .
    uipatapo taarifa hii mfahamishe kiongozi mwenzako
WAKATI AMBAPO WENZETU WAZANZIBAR WAKIFURAHIA KUFUTURISHWA PASI NA SEMINA NA MAKAMU WA KWANZA WA RAISI WA ZANZIBAR MHE.MAALIMU SEIF SHARIFU HAMD NYUMBANI KWAKE MBWENI KAMA PICHA INAVYO ONYESHA HAPO CHINI SISI  HUKU ARUSHA FUTARI MFANO WA HIYO IMEKUWA CHUNGU
  

Sunday, 6 July 2014

Watu 29 wauawa katika shambulizi, Kenya- 6 Julai, 2014



Mashambulizi katika eneo la Mpeketoni kenya
Wizara ya maswala ya ndani nchini Kenya inasema kuwa takriban watu thelathini wameuawa katika mashambulizi mawili tofauti katika makaazi ya pwani ya kenya karibu na mpaka wa Somali.
Watu 20 waliuawa katika eneo la Gamba kaunti ya Tanariver huku tisa wengine wakiuawa kufuatia ufyatulianaji wa risasi katika kituo kimoja cha kibiashara kaunty ya lamu karibu na mpaka wa Somali.
Inadaiwa kuwa watu walikuwa wakitizama mechi za kombe la dunia wakati wa tukio hilo.
Shambulizi la pili lilitekelezwa karibu na eneo la Mpeketoni ambapo zaidi ya watu sitini waliuawa katika shambulizi jengine mwezi uliopita.
Kundi la wapiganaji wa Al shabaab limekiri kutekeleza mashambulizi hayo.
 6 Julai, 2014 - Saa 20:48 GMT
Mashambulizi katika eneo la Mpeketoni kenya
Wizara ya maswala ya ndani nchini Kenya inasema kuwa takriban watu thelathini wameuawa katika mashambulizi mawili tofauti katika makaazi ya pwani ya kenya karibu na mpaka wa Somali.
Watu 20 waliuawa katika eneo la Gamba kaunti ya Tanariver huku tisa wengine wakiuawa kufuatia ufyatulianaji wa risasi katika kituo kimoja cha kibiashara kaunty ya lamu karibu na mpaka wa Somali.
Inadaiwa kuwa watu walikuwa wakitizama mechi za kombe la dunia wakati wa tukio hilo.
Shambulizi la pili lilitekelezwa karibu na eneo la Mpeketoni ambapo zaidi ya watu sitini waliuawa katika shambulizi jengine mwezi uliopita.
Kundi la wapiganaji wa Al shabaab limekiri kutekeleza mashambulizi hayo.

Friday, 4 July 2014

BOMU LINGINE LAJERUHI NYUMBANI KWA SHEIKH

BAADHI YA ASKARI NA RAIYA WAKIWA MAENEO YA TUKIO

 Ni yumbani kwa sheikh sudi mkurugenzi wa taasisi ya kiblaten iliyopo jijini hapa ilikuwa ni majira ya saa 5 usiku baada ya kutoka swala ya taraweh alipo kuwa nyumbani kwake, kama majirani  wanavyo eleza kuwa walisikia mshindo mkubwa wakawa wanazania ni tairi ya gari imepasuka wakati walipotoka nje nakuanza kufuatilia kwa karibu nahatimaye  kufika nyumbani kwa sheikh  sudi ndipo walipokuta  majeruhi wawili sheikh sudi pamoja na mgeni wake ambaye jina lake halijafahamika ndipo wakapiga simu polisi na muda si mrefu rpc pamoja na mkuu wa mkoa waliweza kufika na baadhi ya makamnda ambapo sheikh sudi amejeruhiwa karibu na kiuno na yule mgeni wake amekatwa vidole vya miguu  na hivi sasa majeruhi hao wako katika hospitali ya mkoa ya mount meru na wanaendelea na matibabu ambapo sheikh sudi yeye ametundikiwa dripu ya maji wakati mgeni wake akiwa ametundikiwa dripu ya damu endelea kufuatilia baada ya muda tutakuletea habari kamili na hizi ni baadhi ya picha za eneo husika
    
DILISHA LA NYUMA LILIPO RUSHIWA BOMU HLO


KILA MTU ANASTAAJABU KUTONA NA HALI ILIVYO 

picha ya majeruhi wa bomu wakiwa hospitali ya mkoa wa arusha
Sheikh wa Msikiti wa Qiblatan,Sud Ally Sood (37) uliopo Kilombero jijini hapa amejeruhiwa kwa bomu la kurushwa kwa mkono alipokuwa akila daku nyumbani usiku wa kuamkia jana, mtu mwingine aliyekuwa nyumbani kwake,aliyetajwa kwa jina la Muhaji Kifea (38) mkazi wa Sinza jijini Dar es Salaam pia amejeruhiwa katika tukio hilo na wote wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru kwa matibabu. Sheikh alijeruhiwa miguu yake yote na mapajani huku Kifea akipata majeraha makubwa zaidi miguuni na kupoteza baadhi ya vidole vya miguu yote.

Copyright @ 2014 UWASUWA.

Designed by Japhary | Japhary Juma