Kongamano la Miiraji Tarehe 25/05/2014 saa 2:00 asubuhi Ukumbi wa CCM Mkoa - Arusha. More... Click Here!


Saturday, 24 June 2017

HIVI NDIYO YALIVYO KUWA MASHINDANO YA KUHIFADHI QUR-AN 29/RAMADHA/1438 SAWA NA 24/6/2017

Katika Mashindano hayo yaliyo shirikisha Madrasa nane ( 8 ) za Jijini Arusha mbazo ni Hidaya kutoka Olmatejo,Darul Qur-an kutoka Sombetini, Nuri kutoka Ngarenaro ,Manazilul Abraar kutoka kwa morombo, Arusha Islamic Center kutoka Majengo ,Abdurahmaan Bin Auf kutoka Olmatejo , Swafa kutoka Kaloleleni na wenywji wao  Shamsili Maarif kutoka Shamsi.
KIJANA ABDULHAKIMU MUHAMMAD ALIYE VAA KOFIA NYEUPE NDIYE ALIYE SHIKA NAFASI YA KWANZA KWENYE KUNDI HILI LA JUZUU MOJA NAKUZADIWA SH 50,000/=  ,ANAYE FUATA KATIKATI MTOTO AMANI AYOUB SHIJA ALIIBUKA KUWA MSHINDI WA PILI  NA ALIZADIWA SH 30,000/=NA KIJANA ABDULRAHIMU JUMA (ALOLOO) ALIBUKA KUWA MSHINDI WA TATU NA ALIZAWADIWA SH 20,000/=
Baadhi ya walio hudhuria katika mshindano hayo kama tunavyo waona na miongoni mwao ndio mara ya kwanza kushiriki mashindano ya qur-an hapo anaonekana mwanafunzi Amani Ayoub shija ( mshindi wa pili wa juzuu moja) akiwa ameinamisha kichwa chini akifiria hivi anaweza kufanya vizuri pia ukimtazama mwanafunzi Abdurahimu Juma Aloloo ( mshindi wa tatu wa juzuu moja )  akiwa ameshika mashavu huku akitafakari mchuano namana ulivyo kuwa mkali
Mzee Ally Kassu baada ya kustaafu mashindano ya kuendesha magari ameibukia kwenye mashindano ya kuhifdhi Qur-an na hapo akichukuwa zawadi baada ya kufanya vizuri katika mashindano hayo
Majaji wa masindanano hayo wakijumuisha max baada ya makundi yote manne kusoma aliyeshika kalamu ni Ustadhi Hussein Hassan Myuyi ambae ni katibu wa Umoja wa Walimu Mkoa Arusha anaefuata  ni Ustdhi Gingi anajumuisha max ambaye  ni mmoja miongoni mwa walimu wa kituo maarufu cha kuhifadhisha Quran Jijini hapa kituo cha abdurahmaan bini auf cha hapo olmatejo na anayefuata ni sheikh Hadiyyu Hussein Lukarange ambe yeye ni Naibu Mudiyr wa Markazi ya Azhar Sharif ya Jijini Arusha
kijana mwenye kanzu na kofia nyeupe (Thabiti Salimini) kutoka Shamsil Maarif aliibuka kuwa mshindi wa kwanza wa juzuu tatu na alizawadiwa sh 80,000/= na anae fuata mwenye kilemba chekundu kijana Saadat Abdullahi kitoka Taasisi ya Hidaya Olmatejo alikuwa mshindi wa pili wa juzuu tatu na alizawadiwa sh 50,000/=  na Bw.Mahmudu Sufiyan muendesha bodaboda maarufu wa kijiwe cha Shamsi aliweza kuipokonya nafasi ya tatu na alizawadiwa sh 30,000/=  katika mashindano ambayo yalikuwa na mchuano mkali  katika kundi hilo lililo shirikisha washiriki ishirini na moja (21)

kijana mdogo katikati ( Luqman mohamed ) kutoka kituo cha Abdirahmaan bin Auf  olmatejo Alijinyakulia nafasi ya kwanza na kuzawadiwa sh 100,000/= ,anaye fuatia  Kijana Hambali Hambali Mohamed aliye vaa kofia  kutoka Arusha Islamic Center alichuwa nafasi ya pili na kuzawadiwa sh 80,000/=  na kijana Issa Mohamed kutoka Madrasat Nuri Ngarenaro aliye vaa kilemba kichwani  alishika nafasi ya tatu na kuzawadiwa sh 50,000/=

Mshindi wetu wa kwanza katika kundi hili la juzuu tisa ( 9 ) alikuwa   ni Hamza bin Ally kutoka kituo cha tahfidhul Quran cha Abdurahman bin Auf hapo olmatejo na alizawadiwa sh 150,000/= nafasi ya pili ilichukuliwan na  Binti mdogo aliye vaa hijabu nyeusi ( Hajra bint Rashidi ) kutoka Darul Qur-an sombetini  alizawadiwa sh 100,000/=na nafasi ya tatu ilchukuliwa na Swaumu bint Issa Khamis kutoka shamsil maarif  alye vaa jilbabu rangi ya maziwa na ufito wa rangi ya kijani  naye alizawadiwa sh 80,000/=
Ustadhi Masoud Hussein Salimu aliye shika  microphone ambaye ndiye mratibu mkuu wa mashindano hayo kabla ya ugawaji wa zawadi alielezea kiufupi namna ambayo mashindano yao yanavyozidi kukuwa makubwa mwaka hadi mwaka na kutoa mwito kwa wahisani mbalimbali waweze kujitokeza kudhamini mashindano hayo ,
Naye naibu Mwenyekiti wa Umoja wa walimu Mkoani Arusha Sheikh Juma Haji Mtandaya wapili kutoka upande wa kulia alitoa msisitizo wa kuwa na mchujo kabla ya kufanya mashindano ya Qur-an kwani wako baadhi ya wanafunzi wanaingia kwenye mashindano ili hali ni wabovu hawana vigezo naakatolea mfano wenzetu Dar-es-salaam wao wanafanya mchujo mpaka mara tano hivyo basi anawaomba wanaoandaa mashindano haya ( shamsil maarif  ) mwakani watakapo andaa tena mashindano  wawafanyie mchujo kabla ya kuingia katika mashindano .
             Khalifa Abubakar Saidi aliye shika kichwa akimuwakilisha Sheikh Salimu Mubarack (Sayyid Sujjada ) ndiye alikuwa mgawaji zawadi kwa niaba ya sheikh kwa washindi na washiriki wa mashindano hayo


Sunday, 11 December 2016

SHEREHE ZA MAULIDI MKOANI ARUSHA KIMKOA ZAFANYIKA ARUSHA MJINI

WANAFUNZI WA MADRSA KAMAA ILIVYO KAWAIDA YAO KUTOKANA NA NAMNA WALIVYO FUNDISHWA KUMPENDA MTUME MUHAMMAD ( S.A.W ) WAO HAKUJALI KUPIGWA NA JUA WAO KILCHO WALETA NI MUSIFU MTUME PAMOJA NA KUMUADHIMISHA

BAADHI YA WALIMU WA UWASUWA WAKISHIRIKI KIKAMILIFU KWENYE KUHAKIKISHA KUWA WANAFUNZI WOTE  WANAO HUDHURIA WANAMFURAHIYA MTUME KATIAK HALI SAWA

KATIBU WA UWASUWA AKIWA MSTARI WA MBELE KATIKA ZOEZI LA KUDHIBITI JUA KUTOKANA NA UMATI WA WAISLAMU WA JIJI LA ARUSHA AMBAO KILA BAADA YA DAKIKA CHACHE WALIKUWA WANAONGEZEKA

USTADH ABDILAHI IMAMU WA MSIKITI WA BONDENI AKISOMA DUA YA WASILATU SHAFIY

MGENI RASMI SHEIKH ALLY CHIZENGA AKIWASILISHA MADA YAKE

SHEIKH ISTAMBULI ABDILAHI NAASR AKIWAKILISHA MASHIA WA NCHI YA JIRANI YA KENYA KATIKA MAULIDI HAYO AMBAYO YALIALIKA WATU WOTE

UMOJA WA WALIMU PAMOJA NA KUSIMAMIA BAADHI YA MAMBO WAO KAZI KUBWA WALIYO PEWA NA BARAZA LA BAKWATA ILIKUWA NI KUSIMIA UTARATIBU MZIMA WA KUHAKIKISHA KILA ALIYE HUDHURIA ALITABARUKU HIVYO BASI WALILAZIMIKA BAADHI YAO KUFIKA KWA WAPISHI ILI KUANZA KAZI YAO RASMI NA ALHAMDULILAHI WALISIMAMIA VIZURI

WANAFUNZI WA MADRASA WAKISUBIRI KUHAMISHIWA JUKWAA LA JUU BAADA YA JUA KUWA KALI

NAE SHEIKH ABDURAZAK WA MKOANI HAPA AKIWAKILISHA MASHIA WA ARUSHA KATIKA MAULIDI YA MKOA

BAADHI YA MASHEIKH WA JIJI LA ARUSHA WAKIWA SAFU YA MBELE KAMA TUNAVYO WAONA UPANDE WA KULIA ALIYESIMAMISHA BAKORA YAKE CHINI NI SHEIKH SIMBA KHALFAN AKIFUATIWA NA SHEIKH KISUA ALLY AKIFUATIWA NA MGENI RASMI SHEIKH ALLY CHIZENGA KUTOKA DAR-ES-SALAAM AKIFUATIWA NA SHEIKH WA MKOA WA ARUSHA SHEIKH SHABAN JUMA AKIFUATIWA NA SHEIKH WA WILAYA SHEIKH ABDIRAHMAN SALIM

MWENYEKITI WA UWASUWA USTADHI OMARI SAIDI JOUR AKITAFSIRI BAADHI YA AYA ZA QUR-AN TUKUFU ILIYOSOMWA NA KIJANA OMAR IDDI ABEID

MC.SHEIKH HADIYU HUSSEIN LUKARANGE AKIPITIA RATIBA YAKE ILI KUHAKIKISHA MAMBO YANAKWENDA VIZURI

Saturday, 19 November 2016

KONGAMANO KUBWA LA KIDINI LAFANYIKA MKOA WA ARUSHA LEO 19/11/2016


BAADHI YA KINAMAMA WA KIISLAMU WAKIWA KWENYE KONGAMANO

 KONGAMANO HILI LILIFUNGULIWA KWA QUR-AN TUKUFU ILIYOSOMWA NA SHEIKH MUHAMMAD MAHAMUUDU ABDULFATAAH,
MUDIYRU WA AL-AZHARI SHARIF MKOA WA ARUSHA SHEIKH RAJABU ABDUL HAAD FILFAL AKITOA UFAFANUZI KUHUSU KONGAMANO HILO LILILO KUWA LINA MADA KUU NNE AMBAZO ZILIKUWA ZIKILENGA SUALA ZIMA LA AMANI NA UTULIVU KATIKA JAMII

SHEIKH MKUU WA MKOA WA MANYARA SHEIKH MUHAMMAD KADIDI AKIWASILISHA MADA INAYO HUSU KUTOKUMWAGA DAMU ZISIZO NA HATIA NA ADHABU ATAKAYO PATA MWENYE KUZIPUUZA DAMU  HIZO AKINUKUU AYA KATIKA QUR-AN SURA 5 AYA 32 (MAIDAH)
"Kwa sababu ya hayo tuliwaandikia Wana wa Israili ya kwamba aliye muuwa mtu bila ya yeye kuuwa, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewauwa watu wote. "
NAE MGENI RASMI MHESHIMIWA IDDI HASSAN IDDI KIMANTA MKUU WA WILAYA YA MONDULI AKIMUWAKILISHA MKUU WA MKOAA WA ARUSHA ALIANZA KWA KUPONGEZA SANA KONGAMANO HILO NA KUSISITIZA KUENDELEZA SEMINA NA MAKONGAMANO KAMA HAYO YAFANYIKE MARA KWA MARA KATIKA MAENEO MBALIMBALI YA NCHI YETU

PIA SHEIKH WA WILAYA YA MONDULI SHEIKH MWINSHEE SALIMU NAE HAKUBAKI NYUMA KATIKA KUSISITIZA AMANI YA NCHI, NA KUKEMEA VIKALI KITENDO CHA BAADHI YA WATU KUJICHUKULIA MADARAKA NA MAJUKUMU YASIYO WAHUSU KWANI KUFANYA HIVYO NDIO CHANZO CHA VURUGU NA UVUNJIFU WA AMANI SEHEMU HUSIKA.
SHEUKH RAJABU KIUNGIZA AKIWA NA SHEIKH WA MKOA WA MANYARA WAKIFUATILIA KWA KARIBU KONGAMNO HILO



MUDIYRU WA MARKAZI YA CHANG`OMBE JIJINI DAR ES-SALAAM SHEIKH AWADHI ABDUL-ADHIYMU AKIKABIDHI ZAWADI YA MKUU WA MKOA KWA MKUU WA WILAYA YA MONDULI 

 MKUU WA WILAYA AKITOA SHUKURANI ZA DHATI KWA KUPOKEA ZAWADI KWA NIABA YA MKUU WA MKOA Mh.Mrisho  Gambo
HAWA NI BAADHI YA WAUMINI WAKIWA KWENYE KONGAMANO HILO
MASHEIKH WAKITATHMINI NAMNA KONGAMANO LILIVYO FANA






Friday, 7 October 2016

MASJIDU DARUL MUSTWAFA MTAA WA BONDENI KATA YA TERATI

Moja katika ziyara ambazo wanaendelea nazo UWASUWA ni pamoja na kutembelea msikiti ambao kiwanja husika kilitolewa WAQFU na familia ya .................tunamumba M.Mungu awalipe kila la kheri kutona na nia yao hiyo na pia M.Mungu atuongoze sisi katika kufanikisha malengo ya watoa WAQFU.
مسجد دار المصطفى

HUU NDIO MSIKITI WA DARUL MUSTWAFA KAMA UNAVYOONEKANA KWA MBALI


 BAADHI YA WANAUWASUWA WAKIWA NA WENYEJI WAO NJE YA MSIKITI
HII NI SEHEMU YA NDANI YA MSIKITI

MWENYEKITI WA UWASUWA AKIWA KATIKATI YA WALIMU

MWALIMU ISSA MUHAMMAD AKIHABARISHWA JAMBO NA MWENYEKITI  KUTONA NA MAPOKEZI MAZURI NAMNA WALIVYO POKELEWA NA WENYEJI WAO
HAWA NI BAADHI YA WAUMINI KIJIJINI HAPO

KIKAO MAALUMU AMBACHO AGENDA KUU ILIKUWA NI NAMNA YA KUJENGA MSIKITI HUU AMBAO UMEJENGWA KWA MUDA

BAADHI YA WANAUWASUWA WAKIPOKEA TAARIFA ZA KUFURAHISHA  KATIKA KIKAO BAADA YA KAMATI TEULE KURUDI KATIKA ZIYARA HIYO AMBAYO ILIKUWA NA MAFANIKIO MAKUBWA

WANAUWASUWA WAKIWAZA NAMNA WATAKAVYO FANYA  ILI KUWEZA KUPEANA MAJUKUMU YA KUJENGA MSIKITI HUO
 

Monday, 4 July 2016

MASHINDANO YA KUHIFADHI QUR-AN YALIYO ANDALIWA NA MADRASAT SHAMSIL MAARIF-MKOA WA ARUSHA

KAMA ILIVYO KUWA KAWAIDA YA MADRASAT SHAMSIL MAARIF KILA MWAKA KUANDAA MASHINDANO YA KUHIFADHI QUR-AN MWAKA HUU WALIYAFANYA TAREHE 3/7/2016 SAWA NA RAMADHAN 27/1437









Copyright @ 2014 UWASUWA.

Designed by Japhary | Japhary Juma