Kongamano la Miiraji Tarehe 25/05/2014 saa 2:00 asubuhi Ukumbi wa CCM Mkoa - Arusha. More... Click Here!


Sunday, 26 October 2014

MSIKITI MKUU WA ARUSHA NA MAADHIMISHO YA MWAKA MPYA WA KIISLAAMU 1436 HIJIRIYA

JUMAPILI YA LEO  26/10/2014 SAWA NA 1/MUHARRAM 1436 HIJIRIYA NI SIKU YA FURAHA KWA WAISLAMU WA JIJI LA ARUSHA KWA KUADHIMISHA MWAKA MPYA WA KIISLAMU NDANI YA MSKITI MKUU
Kwa wasio ujua mji huu wa Arusha msikiti huu uko maeneo ya roundabout  katika baraabra kuu itokayo stendi kuu kuelekea   kituo kikuu cha polisi kama inavyo onyesha picha ifutayo




ROUNDABOUT

NA HILI NDILO LANGO KUU LA KUINGILIA MSKITINI AMBAPO MAADHIMISHO YA MWAKA MPYA YALIFANYKA

MC USTADH KHALID MUSTAFA AKIENDELEA KUWAKARIBISHA WAALIKWA BAADA YA MUDIYR WA AL-AZHAR  KUINGIA KWA AJILI YA KUWASILISHA MADA INAYO ELEZEA TUKIO ZIMA LA HIJRA YA MTUME MUHAMMAD (S.A.W)AMBAPO ALIELEZA KIUREFU KAMA TUTAKAVYO KULETE

USTDH MIRAJ KHAMIS AKITOA TAFSRI YA MADA ILIYO WASILISHWA NA MUDIYR SHEIKH RAJABU ALHAD FILYFAL
MUDIYR AKIMLAKI RAFIKI YAKE ALHAJ SHEIKH RAJABU KIUNGIZA
SEHEMU YA KINABABA WAKIFUATILIA MADA ZINAZO TOLEWA
HAWA NI KINAMAMA AMBAO HAKUBAKIA NYUMA KATIKA KONGAMANO HILO

HII NI SEHEMU YA NDANI YA MSIKITI SIKU YA MAADHIMISHO YA MWAKA MPYA
ENDLEA KUFUATILIA BLOG HII PUNDE TU TUTAKULETEA HABARI KAMILI......


HII NDIYO ILE PAKING YA MAARI AILIYO SEHEMU YA KIBLA


SHEIKH RASHID KUTOKA ZANZIBAR ALIYE NYOOSHA MKONO AKIANZA KUTOA UTANGULIZI WA MADA KUHUSINA NA KALENDA YA HIJRA ILI MUDIYR AJE AKAMILISHE MADA HIYO 


SHEIKH RAJABU KIUNGIZA YEYE KTK KONGAMANO HILI ALIWASILISHA MADA  ILIYOKUWA INASEMA WAISLAMU LAZIMA TUBADIILIKE KILA TUNAPO MALIZA MWAKA LAZIMA TUANGALIE MWAKA ULIOPITA TUMETANGULIZA NINI ALAIZIDI KWENDA MBALI ZAIDI PALE ALIPO SEMA..................................................
HII NI SEHEMU YA NYUMA YA MSIKITI MKUU


HILI NI JENGO AMBALO IKO SHULE YA SEKONDARI YA BONDENI SHULE AMBAYO ILIKUWA KTK SAKRATIL MAUTI KUTOKANA NA HILA ZA MAWABI NA LENGO KUBWA ILIKUWA NI KUIUA KWASABABU WASISI WAKE SI MAWABI 



NAIBU KATIBU WA UWASUWA AKISOMA RISALA PEMBENI YA MGENI RASMI BW.ABDALLAH MASOUD

MUWEKA HAZINA WA UWASUWA AKITOA TAMKO LA SHUKRANI KWA NIYABA YA MWENYEKITI KWA WOTE WALIO HUDHURIA NA KWA UONGOZI WA BAKWATA KUWARUHUSU KUUTUMIA MSKITI HUO KWA AJILI YA KONGAMNO LAO



SEHEMU YA NJE YA SEKONDARI YA BONDENI NA MADRASATIL AZHAR

Monday, 20 October 2014

MTUHUMIWA WA UGAIDI NA KUMWAGIA VIONGOZI WA DINI TINDIKALI AUWAWA MAENEO YA KISONGO-JIJINI ARUSHA

  الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُم مُّصِيبَةٌ قَالُوا إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ

kuzisha hati
Mshukiwa mkuu wa mashambulio ya kigaidi yaliyokuwa yakifanyika  katika mji wa Arusha  ameuawa baada ya kufyatuliwa risasi kadhaa na askari polisi baada ya kujaribu kuruka kwenye gari chini ya ulinzi mkali wa Polisi akisafirishwa kuelekea kwao kondoa kwa ajili ya kuonyesha mabomu mengine aliyo kuwa ameyaficha huko, Taarifa kutoka  kwa kamnda wa Polisi Arusha ndugu Lebaratus Sabas zinasema kuwa, Yahya Omar Hassan Hela maarufu kwa jina la 'Yahya Sensei' ambaye inadai alikuwa mpangaji na mratibu wa mashambulio ya kigaidi mjini Arusha, ameuawa kwa kupigwa risasi wakati alipojaribu kuruka kwenye gari la polisi kwa lengo la kuwatoroka. Jeshi la Polisi limeeleza  kuwa, mtuhumiwa huyo alikiri kuhusika na upangaji na uratibu wa mashambulio tisa ya kigaidi katika miji ya Arusha, Zanzibar, Mwanza na Dar es Salaam wakati alipohojiwa na jeshi hilo.
Miongoni mwa mashambulio yaliyofanywa na mtuhumiwa huyo ni lile lililofanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph  lililopo Olasiti jijini Arusha, lililosababisha vifo vya watu watatu na majeruhi 36.

                      

              

Wednesday, 15 October 2014

Vvitisho vya Marekani dhidi ya Mataifa mengine vyakosolewa

Mhadhiri na msomi mashuhuri nchini Marekani ndugu Arvam Noam Chomsky
 amewakosoa vikali viongozi wa Marekani kwa kutoa matamshi ya vitisho dhidi ya Iran. Akihojiwa na Press TV mjini New York, Noam Chomsky amesema kuwa, wanadiplomasia wa Magharibi na hasa Marekani wanatoa matamshi ya vitisho dhidi ya Iran na hata wanathubutu kusema kwamba, chaguo la kutumia njia za kijeshi bado liko mezani, katika hali ambayo utumiaji wa lugha za vitisho dhidi ya nchi nyingine ni ukiukwaji wa sheria za kimataifa. Msomi huyo mashuhuri nchini Marekani ameongeza kuwa, matamshi hayo ya vitisho yanayotolewa na viongozi wa Marekani kuhusiana na miradi ya nyuklia ya Iran yenye malengo ya amani yanaweza kutafsiriwa kwamba Washington inaweza kutumia nguvu za kijeshi dhidi ya Iran. Marekani na baadhi ya washirika wake wa Ulaya mara kadhaa wamekuwa wakiituhumu Iran kwamba miradi yake ya nyuklia ina malengo ya kijeshi. Inafaa kuashiria hapa kuwa, viongozi wa ngazi za juu wa Iran wamesisitiza mara kadhaa kuwa, Iran kamwe haina mpango wa kutengeneza kombora la atomiki, kwani mpango huo unakinzana na misingi ya sheria za dini tukufu ya Kiislamu.

Saturday, 11 October 2014

KUNA NINI LEO KWA WANAFUNZI SEKONDARI YA URAKI NA LEKI TATU

Ni furaha zisizo elezeka kwa wanafunzi wa kiislamu wa shule hizo mbili walipo amua kuungana pamoja katika mahafali yaliyo fanyika Sekondari ya Uraki
SEHEMU KTK JUKWAA KUU LINAONEKANA LIMEPAMBWA NA BAADHI YA  WAGENI WAALIKWA






M.C MWALIMU ABUSHAKUR MUSTAFA ANA WAKARIBISHA WOTE WALIHUDHURI MAHAFALI HAYA KWA KUSEMA KUWA MGENI RASMI NDIO ANAINGI  HIVYO KILA ALIYE MBALI ASOGEE NA ACHUKUWE NAFASI YAKE KWA SABABU TUKO NJE YA WAKATI .FUNDI MITAMBO PIA HAKUCHEZA MBALI NA KAZI YAKE KAMA TUNAVYO MUONA



BAADA YA MC KUTOA TANGAZO LAKE KINABABA WALIWAHI NAFASI ZAO KAMA TUNAVYOONA

 
Kwa upande wa kina mama pia hawakubaki nyuma kwani wao ndio walionyesha kuwa na kiu zaidi katika mahafali haya ya mwaka wa nne.
      Baada ya kuwa watu wamekaa na kutulia mahafali yetu yalianzwa kwa dua ilombwa na mzee wetu mzee Amani kutoka masjidi majengo kufutiwa na Qur-an tukufu iliyo somwa na Amiri wa wanafunzi Leki tatu Ustadh Kisra Juma
        Ambpo mufasiri wa aya zilizo somwa alikuwa ni Sheikh Miraji Khamis  kutoka Masjid Taqwa
wa mjini Arusha ambapo alizama zaidi ktk aya hizi tatu zinazo sema:-
-                                                            إِنَّ لِلْمُتَّقِينَ مَفَازًا ﴿٣١﴾ حَدَائِقَ وَأَعْنَابًا ﴿٣٢﴾ وَكَوَاعِبَ أَتْرَابًا ﴿٣٣﴾     د 
       Na baada ya kutafiriwa aya hizo ilifutia mada ya kwanza ambayo iliwasilishwa na Imamu wa msikiti wa majengo mada ambayo ili beba mambo makuu mawili jambo lakwanza ilikuwa ni kuhusiana na Wazazi ,wazazi wanao wajibu wa kuzidi kuwasomesha watoto wao elimu zote Elimu ya Dinii kwa ajili ya akhera yao na elimu ya dunia kwa ajili ya duia yao na jambo la pili lili wahusu wanafunzi na zaidi sheikh alihimiza kuhusiana an adabu.
            Ambapo mada ya pili iliwasilishwa na Ustadh Masoud Hussein kutoka masjid Mahfuudh Mtaa wa shamsi mjni Arusha na na yeye alielezea uislamu namna  ulivyo himiza kuhusina na kutafuta elimu na alianza na aya ambazo zilisomwa na msomaji Qur-an wa pili katika mahafalia hayo Amir wa shule ya Uraki kijana Hamad Kundya aya ambazo zilikuwa ni zakwanza kushushwa katika Quran kwa mtume wetu muhammad ( s.a.w ) yaani katika surat alaq :-

اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ ﴿١﴾ خَلَقَ الْإِنسَانَ مِنْ عَلَقٍ ﴿٢﴾ اقْرَأْ وَرَبُّكَ الْأَكْرَمُ ﴿٣﴾ الَّذِي عَلَّمَ بِالْقَلَمِ ﴿٤﴾ عَلَّمَ الْإِنسَانَ مَا لَمْ يَعْلَمْ ﴿٥﴾
           Ambapo mada ya mwisho iliwasilishwa na sheikh Abdurahman Idrisa imamu wa masjid Irshad Ngarasero ambapo yeye alizama katika mashairi baada ya kuona mada ya kwanza ilizama ktk hadith na mada ya pili ktk Qur-an na zaidi aliamua kumuelezea msomi kwa kusema msomi ni mtu hatari sana endapo ataitumia elimu yake vibaya na upande wa pili msomi ni mtu mwenye manufaa sana endapo ataitumia elimu yake vizuri.
             Baada ya mada ya mwisho ilisomwa risala na mmoja ktk wahitimu wa kidato cha nne risala ambayo ilbeba ujumbe mzito unahusiana na taaluma ya kiislamu mashuleni ,upotevu wa maadili ya mavazi kwa wanafunzi wakike na uhaba wa nyenzo na hasa vitabu vya marifa ya uslamu ambpo seti moja ni shilingi elfu thelathini tu.
MGENI RASMI BWANA OMARY MSHANA KIBIDHIWA RISALA NA MSOMA RISALA NA BAADA YA RISALA UTOAJI VYETI ULIANZA KAMA TUNVYO ONA KTK TUKIO LINALO FUATA
MUHITIMU WA KIDATO CHA NNE BAADA YA ZAWADI

Baada ya ugawaji vyeti ulisomwa dua ya kufunga mahafali hayo na Mzee Amani mnamo majira ya asaa 1:15 watu wote walitakiwa waingie kwenye ukumbi wa chakula na baada ya hapo kila mmoja aliruhusiwa na hapo ndi mwisho wamahafali ya mwaka huu wa 2014










Copyright @ 2014 UWASUWA.

Designed by Japhary | Japhary Juma