Kongamano la Miiraji Tarehe 25/05/2014 saa 2:00 asubuhi Ukumbi wa CCM Mkoa - Arusha. More... Click Here!


Saturday, 9 August 2014

Marekani yaendeleza mashambulizi Iraq


10 Agosti, 2014 - Saa 02:52 GM


Mashambulizi ya marekani

Marekani imesema kuwa imetekeleza mashambulizi zaidi kazkazini mwa Iraq dhidi ya maeneo yanayodhibitiwa na wapiganaji wa Jihad.
Taarifa kutoka Pentagon imesema kuwa ndege za Marekani pamoja na zile zisizo na rubani ziliharibu magari ya kijeshi ya wanamgambo hao likiwemo lile lilokuwa likiwashambulia raia wa Yazidi ambao wamekimbilia hifadhi katika mlima Sinjar.
Awali Rais Obama amesema kuwa kupitia washirika wake wa ulaya pamoja na wanajeshi wa Iraq watawakabili wanamgambo ambao wameuzunguka mlima huo.
Hatahivyo ameonya kuwa kampeni hiyo ya kijeshi itachukua miezi kadhaa na kwamba itachukua mda kwa jeshi la Iraq kujikusanya ili kutoa upinzani mkali dhidi ya wanamgambo hao.

Ndege za marekani zilizobeba misaada nchini Iraq
Wakati huohuo Ndege za kijeshi za Marekani na zile za Uingereza zimeendelea kuangusha misaada kwa raia waliokwama katika Mlima Sinjar nchini Iraq,ijapokuwa viongozi wa mataifa hayo mawili wamekubaliana kwamba hatua hiyo sio suluhu ya kudumu.
Wamesema kuwa lazima njia ya kuwaondoa raia hao hadi katika eneo lililo salama itafutwe ili kuzuia mauaji ya kimbari.
Mfanyikazi mmoja wa shirika la Amnesty International kazkazini mwa Iraq, Donatella Rovera ameiambia BBC kwamba maelfu ya raia kazkazini na magharibi mwa mlima huo wamefanikiwa kutoroka,lakini wengi zaidi katika eneo la kusini la mlima huo hawana mahala pa kwenda.
Amesema kuwa wale waliotoroka wako katika hali mbaya baada ya kukaa siku sita bila chakula na maji kidogo.

USA:Hatutakubali uongozi wa Khalifa Iraq


 9 Agosti, 2014 - Saa 11:37 GMT
Ndege za kijeshi za marekani
Rais Obama amesema kuwa hatakubali wapiganaji wa Kisunni kubuni taifa la kiislamu katika maeneo inayodhibiti ndani ya mataifa ya Syria na Iraq.
Obama alikuwa akizungumza katika mahojiano na gazeti la New York times baada ya marekani kutekeleza mashambulizi ya angani dhidi ya wanamgambo wa ki-suni ambayo amesema yalikuwa muhimu ili kuulinda mji wa kikurdi wa Irbil
Obama amesema kuwa marekani ina maslahi yake katika kuyazuia makundi ya wanamgmbo mbali na kusitisha mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa dini zilizo na wachache.
Wakati huohuo Rais Obama amesema kuwa hatakubali wapiganaji wa Kisunni kubuni taifa la kiislamu katika maeneo inayodhibiti ndani ya mataifa ya Syria na Iraq.
Obama alikuwa akizungumza katika mahojiano na gazeti la New York times baada ya marekani kutekeleza mashambulizi ya angani dhidi ya wanamgambo wa ki-suni ambayo amesema yalikuwa muhimu ili kuulinda mji wa kikurdi wa Irbil.
Obama amesema kuwa marekani ina maslahi yake katika kuyazuia makundi ya wanamgmbo mbali na kusitisha mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa dini zilizo na wachache.

Friday, 8 August 2014

CAR kuunda mahakama maalumu ya jinai

Serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati itaunda mahakama maalumu itakayochunguza jinai zilizofanyika katika nchi hiyo iliyoathiriwa na vita vya ndani. Mwanasheria Mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Ghislain Grésenguet amesema kuwa mahakama hiyo maalumu itachunguza na kutathmini jinai zilizofanyika nchini humo katika vita vya ndani. Amesema kamati ya wanasheria 8 inapitia nyaraka za awali za kunzishwa mahakama hiyo na itaanza shughuli zake wiki ijayo. Awali Rais Catherine Samba- Panza wa Jamhuri ya Afrika ya Kati alikuwa ameitaka Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) yenye makao yake nchini Uholanzi kushughulikia faili la jinai zilizofanyika nchini humo. Maelfu ya watu wengi wao wakiwa Waislamu wameuawa na malaki ya wengine kukimbia makazi yao katika mashambulizi ya kundi la Kikristo la Anti Balaka dhidi ya Waislamu walio wachache katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Waislamu Myanmar wangali katika hali mbaya


 Waislamu wa jamii ya Rohingya nchini Myanmar wangali wanaishi katika hali ngumu na mazingira mabaya na makumi ya maelfu miongoni mwao wanakabiliwa na uhaba wa chakula, maji na huduma za afya. Ripoti zinasema kuwa serikali ya Myanmar imeendeleza sera zake za ubaguzi dhidi ya Waislamu kwa kuzuia jumuiya za kimataifa za misaada ya kibinadamu kuingia katika maeneo ya Waislamu wa jamii ya Rohingya. Mwandishi wa Press TV anaripoti kuwa kambi za wakimbizi wa Kiislamu wa Rohingya hazina huduma za afya, maji na mahitaji mengine ya dharura na kwamba serikali ya Myanmar inabana shughuli za jumuiya za misaada ya kibinadamu kwa wakimbizi hao. Maelfu ya Waislamu wa jamii ya Rohingwa wanaounda asilimia tano ya watu wa Myanmar wameuawa na maelfu ya wengine kukimbia makazi yao kufuatia mashambulizi yanayofanywa na Mabudha wenye misimamo mikali wanaosaidiwa na jeshi la serikali. Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa Waislamu wa Rohingya wa Myanmar ni miongoni mwa jamii zilizodhulumiwa zaidi duniani.

Thursday, 7 August 2014

Anti Balaka wamekiuka makubaliano ya amani CAR'

Magaidi wa Anti-Balaka Msemaji wa Mungano wa Seleka katika Jamhuri ya Afrika ya Kati amesema kuwa, hatua ya kundi la Kikristo la Anti Balaka ya kuyaunga mkono majeshi ya Ufaransa dhidi ya wanamgambo wa Seleka inakinzana na makubaliano ya amani yaliyofikiwa hivi karibuni huko Brazzaville, Jamhuri ya Kongo. Djouma Narkoyo amesema kuwa, majeshi ya Ufaransa yakipata uungaji mkono wa Anti Balaka yalifanya mashambulio dhidi ya wanamgambo wa Seleka na kuua wapiganaji wasiopungua 50 huko kaskazini mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati. Taarifa zinasema kuwa, mapigano hayo yamejiri masaa machache tu baada ya Andre Nzapayeke Waziri Mkuu wa nchi hiyo kujiuzulu wadhifa huo. Wakati huohuo, Rais Catherine Samba –Panza wa Jamhuri ya Afrika ya Kati ameanza kufanya mazungumzo na wawakilishi wa makundi mbalimbali kwa lengo la kumteua Waziri Mkuu mpya wa serikali ya mpito. Rais Samba –Panza ameeleza matumaini yake kwamba, Waziri Mkuu mpya atachaguliwa kufikia wiki ijayo.

Tuesday, 5 August 2014

Waziri mwandamizi ajiuzulu Uingereza

Sayeeda Warsi  amejiuzulu  wadhifa  wake  wa  waziri mwandamizi  katika  wizara  ya  mambo  ya  kigeni  ya Uingereza  leo, akisema  kuwa  hawezi  tena  kuunga mkono  sera  za  serikali  hiyo  kuhusiana  na  mzozo  kati ya  Israel  na  Hamas. Warsi , amekuwa  Muislamu  wa kwanza  katika  baraza  la  mawaziri  wa  Uingereza  mwaka 2010  lakini  baadaye  alishushwa  cheo  na  kuwa  waziri mwandamizi  katika wizara  ya  mambo  ya  kigeni  na waziri  wa  masuala  ya kidini  na  jamiii.

Marekani yatoa kauli mbiu za ghiliba kwa Waafrika

Marekani yatoa kauli mbiu za ghiliba kwa Waafrika

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani John Kerry kabla ya kuanza kikao cha pamoja cha viongozi wa Afrika na Marekani mjini Washington amedai kwamba, serikali ya Washinton inashikamana kikamilifu na thamani na misingi ya demokrasia na utetezi wa haki za binadamu.
Akizungumza mbele ya wanaharakati wa jamii na makundi ya kiraia hapo jana, Kerry ametaka ziimarishwe asasi na taasisi mbalimbali barani Afrika badala ya kuimarishwa nguvu za viongozi wa Kiafrika na kusisitiza kwamba, Washington inaunga mkono ukomo wa mihula miwili ya uongozi kwa marais katika nchi za Kiafrika. John Kerry amewataka viongozi wa Kiafrika kutobadili katiba kwa ajili ya maslahi yao binafsi au ya kisiasa.
Nara na kauli mbiu za ghiliba na hadaa za uungaji mkono wa misingi ya haki za binadamu za Marekani zinatolewa na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa nchi hiyo katika hali ambayo, utawala wa Kizayuni wa Israel unaendelea kufanya mauaji na jinai za kivita na zilizo dhidi ya binadamu dhidi ya wananchi wa Palestina wa Ukanda wa Ghaza kwa kupata uungaji mkono wa moja kwa moja na misaada ya fedha na silaha ya Marekani. Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch limetangaza kuwa, mauaji dhidi ya wananchi wa Ghaza ni jinai za kivita na limetaka mashambulio ya majeshi ya Israel dhidi ya wananchi wa Ghaza yakomoshwe haraka iwezekanavyo.
Kikao cha pamoja cha siku tatu cha viongozi wa Afrika na Marekani kilianza jana mjini Washington lengo kuu likiwa ni kuimarisha uhusiano unaozidi kuyumba kati ya Marekani na nchi za Kiafrika.
       Habari hii kwa hisani ya idahaa ya kiwsahili ya redio tehran

Copyright @ 2014 UWASUWA.

Designed by Japhary | Japhary Juma