Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani John Kerry kabla ya kuanza kikao cha pamoja cha viongozi wa Afrika na Marekani mjini Washington amedai kwamba, serikali ya Washinton inashikamana kikamilifu na thamani na misingi ya demokrasia na utetezi wa haki za binadamu.
Akizungumza mbele ya wanaharakati wa jamii na makundi ya kiraia hapo jana, Kerry ametaka ziimarishwe asasi na taasisi mbalimbali barani Afrika badala ya kuimarishwa nguvu za viongozi wa Kiafrika na kusisitiza kwamba, Washington inaunga mkono ukomo wa mihula miwili ya uongozi kwa marais katika nchi za Kiafrika. John Kerry amewataka viongozi wa Kiafrika kutobadili katiba kwa ajili ya maslahi yao binafsi au ya kisiasa.
Nara na kauli mbiu za ghiliba na hadaa za uungaji mkono wa misingi ya haki za binadamu za Marekani zinatolewa na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa nchi hiyo katika hali ambayo, utawala wa Kizayuni wa Israel unaendelea kufanya mauaji na jinai za kivita na zilizo dhidi ya binadamu dhidi ya wananchi wa Palestina wa Ukanda wa Ghaza kwa kupata uungaji mkono wa moja kwa moja na misaada ya fedha na silaha ya Marekani. Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch limetangaza kuwa, mauaji dhidi ya wananchi wa Ghaza ni jinai za kivita na limetaka mashambulio ya majeshi ya Israel dhidi ya wananchi wa Ghaza yakomoshwe haraka iwezekanavyo.
Kikao cha pamoja cha siku tatu cha viongozi wa Afrika na Marekani kilianza jana mjini Washington lengo kuu likiwa ni kuimarisha uhusiano unaozidi kuyumba kati ya Marekani na nchi za Kiafrika.
Habari hii kwa hisani ya idahaa ya kiwsahili ya redio tehran
0 comments:
Post a Comment