Kongamano la Miiraji Tarehe 25/05/2014 saa 2:00 asubuhi Ukumbi wa CCM Mkoa - Arusha. More... Click Here!


Saturday, 9 August 2014

Filled Under:

Hali ya usalama inayotawala nchini Iraq hivi sasa

kuzisha hati

Sisitizo la maulama kadhaa na wananchi wa miji mbalimbali ya Iraq juu ya umoja wa kisiasa na kuwekwa kando tofauti, kuahirishwa kikao cha bunge kwa ajili ya kuchaguliwa kundi kubwa zaidi la wawakilishi bungeni ambalo litakuwa na jukumu la kumteua Waziri Mkuu, hadi Jumapili ijayo, kuendelea jinai za kigaidi za kundi la Daesh kwa kushirikiana na mabaki ya utawala wa Kibaath na kuendelea mapigano kati ya jeshi na makundi ya kigaidi, ni matukio muhimu zaidi yaliyotawala hivi hivi sasa jamii ya Iraq.
Abdul Mahdi al Karbalai, mwakilishi wa Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Sistani, alimu mkubwa na marjaa wa kidini wa Waislamu wa madhehebu ya Kishia katika mkoa wa Karbala, amewataka wananchi kuimarisha umoja wao na kushirikiana na jeshi la nchi hiyo katika mapambano dhidi ya makundi ya kigaidi na kitakfiri nchini humo. Akiashiria juu ya umuhimu wa vyama vya siasa kuiunga mkono serikali na jeshi katika vita vyake dhidi ya magaidi amesema kwamba, kuna udharura wa kuweka kando tofauti za mitazamo na kuunganisha nguvu kwa ajili ya kupambana na ugaidi wa kitakfiri, hasa katika kipindi hiki ambacho kundi la Daesh limezidisha harakati zake za uharibifu na mauaji nchini humo.
Kwa upande wake, Wisam al Hardan, mkuu wa kongresi ya mwamko nchini Iraq amesema kuwa, maulama wa Kisuni wanatakiwa kuchukua hatua madhubuti katika kukabiliana na jinai za magaidi, sambamba na kutangaza kujibari kikamilifu na vitendo hivyo. Ameongeza kwa kusema kuwa, magaidi wa Daesh wanatumia kila suhula kwa ajili ya kutoa pigo kwa  Waislamu na Uislamu kwa ujumla, hivyo yeyote yule ananyamazia kimya jinai hizo, ni wajibu wake kutoa maelezo kwa hatua yake hiyo. Kabla ya hapo pia maulamaa 14 wa Kiislamu wa madhehebu ya Kisuni mjini Mosul, walikuwa wametangaza kujitenga kwao kikamilifu na vitendo vya kundi la kigaidi la Daesh mjini hapo. Kwengineko maelfu ya Waislamu katika mkoani Karbala walifanya maandamano makubwa hapo juzi Alkhamisi wakimuunga mkono Waziri Mkuu wa Iraq, Nouri al Maliki. Washiriki wa maandamano hayo walitangaza nia yao ya kutaka Nouri al Maliki achaguliwe kwa mara ya tatu kushika nafasi hiyo ya Waziri Mkuu. Wadhah Salim al Tamimi, mmoja wa waandaaji wa maandamano hayo alisema kuwa, kuna umuhimu wa muungano wa kitaifa nchini Iraq kuunda serikali chini ya uongozi wa Nouri al Maliki. Mbali na Karbala, maandamano kama hayo yameshuhudiwa pia katika mkoa wa Dhi Qar, kusini mwa Iraq, ambapo waandamanaji wametangaza kumuunga mkono waziri mkuu huyo. Hayo yanajiri wakati ambao baada ya kutofanikiwa vikao viwili vya bunge vilivyokuwa na lengo la kuchaguliwa kundi kubwa zaidi la wawakilishi bungeni, bunge hilo limeamua kuahirisha kikao hicho hadi siku ya Jumapili. Kwa mujibu wa katiba ya Iraq, mrengo huo mkubwa wenye wabunge wengi, utakuwa na juku la kumchagua waziri mkuu wa nchi hiyo.
Kwa upande wa usalama, mapigano kati ya jeshi la serikali na wanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh, yameendelea kuripotiwa katika maeneo kadhaa ya nchi hiyo. Duru za kuaminika zimeripoti kuwa karibu watoto 300 wa kabila la Yazidi wamepoteza maisha yao katika kipindi cha masaa 48 yaliyopita, kutokana na kukosa chakula na maji ya kunywa. Wakati huo huo Khadir al Mahna, mmoja wa wajumbe wa Baraza la Mwamko katika mkoa wa Diyala, mashariki mwa Iraq, amesema kuwa, kundi la Daesh mjini Baqubah na Mosul limekuwa likiwatumia watoto wadogo katika vitendo vya kigaidi. Weledi wa mambo wanaamini kuwa, kuchaguliwa waziri mkuu wa Iraq kutatoa pigo kwa makundi ya kigaidi na waungaji wao mkono wasioitakia heri nchi hiyo

0 comments:

Post a Comment

Copyright @ 2014 UWASUWA.

Designed by Japhary | Japhary Juma