Matifa ya kiarabu (Arab League)yameanza kupinga kuingiliwa Nchi ya Libya na matifa ya kigeni
Akijibu ombi la bunge la Libya kwa
Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuingilia kijeshi nchini humo ili
kuwalinda raia na kukabiliana na makundi ya wanamgambo, Fadhil Muhammad,
Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu amesema kuwa jumuiya
hiyo haiidhinishi uingiliaji wa nchi za kigeni huko Libya na kwamba
inaamini kuwa nchi za Kiarabu zenyewe zinapaswa kutatua matatizo yake
ili kusiwepo na haja ya uingiliaji wa wageni.
Naibu Katibu Mkuu wa Arab League
ameongeza kuwa, jumuiya hiyo inatiwa wasiwasi na matukio yanayojiri huko
Libya na kwamba inasikitishwa na mapigano na machafuko ya umwagaji damu
yanayoendelea kati ya makundi yenye silaha nchini humo. Fadhil Muhammad
amesema anatumai kwamba bunge la Libya litaweza kurejesha amani na
utulivu nchini humo kwa kusaidiwa na nchi jirani na zile za Kiarabu
Wednesday, 20 August 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment