Sayeeda Warsi amejiuzulu wadhifa wake wa waziri
mwandamizi katika wizara ya mambo ya kigeni ya
Uingereza leo, akisema kuwa hawezi tena kuunga
mkono sera za serikali hiyo kuhusiana na mzozo kati
ya Israel na Hamas. Warsi , amekuwa Muislamu wa
kwanza katika baraza la mawaziri wa Uingereza mwaka
2010 lakini baadaye alishushwa cheo na kuwa waziri
mwandamizi katika wizara ya mambo ya kigeni na
waziri wa masuala ya kidini na jamiii.
0 comments:
Post a Comment