Katibu mkuu wa jumuiya ya mataifa ya kiarabu Arab League , Nabil al-Arabi leo ameunga mkono uteuzi wa waziri mkuu mpya wa Iraq Haidar al-Arabi na kujiunga na sauti zinazotolewa kimataifa kuidhinisha kumuweka kando waziri mkuu anayeondoka madarakani Nuri al-Maliki. Al- Maliki ambae sera zake za mtengano zimelaumiwa kwa kuchangia kuchukuliwa kwa maeneo kadhaa ya ardhi na wapiganaji wa kijihadi wa kundi la Dola la Kiislamu, amesisitiza kuwa ni waziri mkuu halali.
Wakati huo huo wachunguzi wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua za haraka kuepusha mauaji ya halaiki dhidi ya jamii ya Wayazidi nchini Iraq.
Makao makuu ya kanisa katoliki linawataka viongozi wa dini ya Kiislamu kushutumu mauaji ya kinyama yanayofanywa na wapiganaji wa taifa la Kiislamu dhidi ya jamii ya Wakristo na makundi mengine ya wachache nchini Iraq.
0 comments:
Post a Comment