Kongamano la Miiraji Tarehe 25/05/2014 saa 2:00 asubuhi Ukumbi wa CCM Mkoa - Arusha. More... Click Here!


Friday, 15 August 2014

Filled Under:

Khatami: Iran haitakubali ubeberu wa Marekani

 kuzisha hati
Khatibu wa Swala ya Ijumaa mjini Tehran amesema kuwa, madhali Marekani ingali inaendeleza uadui na viongozi wake wangali wanatoa matamshi ya kiadui dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kushirikiana na Washington hakuna maana yoyote.
Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami amesema hayo mbele ya hadhara kubwa ya waumini waliohudhuria ibada ya Swala ya Ijumaa mjini Tehran na kusisitiza kwamba, Marekani haifuatilia mazungumzo bali inachotaka ni kuwa na satua na udhibiti kwa taifa hili la Kiislamu. Khatibu wa Swala ya Ijumaa mjini Tehran amesema bayana kwamba, viongozi wa Marekani wanapaswa kuelewa kwamba, mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu na wananchi wa taifa hili katu hawatakubali ubebeberu wa Washington.
Ayatullah Khatami ameashiria kuongezeka matarajio na vikwazo vya Wamarekani katika mwenendo wa mazungumzo ya nyuklia ya hivi karibuni na kusema kuwa, viongozi wa Marekani hawaaminiki, wanatafuta visingizio na katu hawana nia ya kuyapatia ufumbuzi matatizo yaliyopo. Ameashiria pia matukio ya hivi karibuni nchini Iraq na kusisitiza juu ya udharura wa kulindwa umoja na mshikamano wa taifa hilo.
Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Ayatullah Ahmad Khatami amesema kuwa, kundi la kigaidi la Daesh ni natija ya siasa chafu za Magharibi huko Iraq.

0 comments:

Post a Comment

Copyright @ 2014 UWASUWA.

Designed by Japhary | Japhary Juma