Kongamano la Miiraji Tarehe 25/05/2014 saa 2:00 asubuhi Ukumbi wa CCM Mkoa - Arusha. More... Click Here!


Friday, 1 May 2015

MUHADHARA MKUBWA WAFANYIKA ARUSHA

Umoja wa Walimu wa Ahls-Sunna Wal jamaa Arusha ( UWASUWA ) Jana jioni 29/4/2015 katika msikiti mkuu wa ijumaa  ngarenaro al maarufu kwa sheikh mahmuud Salim ulifanya muhadhra ulio simamiwa na walimu wanosomesha dini mkoani hapa ambapo mada teule zilikuwa ni mbili.


Walimu wa Madrasa baada yakuona maswali yamekuwa mengi kuhusu Maulidi ya Mtume Muhammad (s.aw.) kwamba inafaa kuadhimisha au haifai kuadhimisha, na badhi ya waumini kuuliza juu M.Mungu kwamba yuko wapi kwakutatizwa kwao na tafri ya juu juu ya inayo tolewa na baadhi yetu tafsiri ya  sura iliyo teremshwa makkah sura ya 45 kuteremshwa sura yenye aya 135 matamko 1641 herufi 5242 kwa mpangilio wa msahafu ni sura ya 20 aya ya 5 yenye kujulikana kwa jina la surat twaahaa kama tunavyo iyona aya hiyo      ( الرَّحْمَنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَى )
   " Arrahmani, Mwingi wa Rehema, aliye tawala juu ya Kiti cha Enzi "Qur-an 20:5
Ili walazimu UWASUWA kutekeleza majukumu yao katika jamii ya kiislamu kwa kufanya muhadhara wenye mada kuu mbili mada ya maulidi na mada ya tawhidi ambapo mada ya maulidi ili wasilishwa na mwenyekiti wa UWASUWA ustsdh OMARY SAIDI JOUR kutoka Taasisi ya Hidaya Olmatejo  na mada ya tawhidi iliwasilishwa na katibu idara ya Da'awa ustadh Hussein suleyman auf kutoka Taasisi ya Tarbiyatil ilsaam Jr
Mwenyekiti wa UWASUWA  akiwasilisha mada yake kuhusu kufaa kumuadhimisha Mtume ( s.a.w ) mada ambayo nukuu zake nyingi ilikuwa ni kutoka kwa watu walio ishi na Mtume ( Maswahaba ) namana walivyo msifu Mtume ( s.a.w ) , na nukuu nyingine zikitoka kwa wanazuoni wakubwa wa kiislamu namna walivyo elezea kufaa kumsifu bwana Mtume unaweza pia kuzisikiliza mada hizo kupitia Chanel yetu ya youtube.


Baadhi ya waumini wakiwa katika muhadhara huo wakipata faida mbalimbali juu ya kumsifu Mtume (s.a.w )


Ustadh Jabir  Muhammad na Ustadh Miraj Khamis  wakijaribu kurekodi mada kupitia simu zao za mkoni kama wanavyo onekana katika safuhii  ya mbele.



Baada ya mada ya kwanza kukamililika MC wa Muhadhara huo Ustadh Athuman Hussein al marufu kwa jina la Msingidaa alimkaribisha mtoa mada wa pili Ustadh Auf kama tunavyo muona akiweka bidhaa zake mfukoni kwa ajili ya kusima ili kwasilisha mada yake inayo usiana na Tawhidi.

 Katibu Idara ya Da'awa Ustadh Auf  akiwasilisha mada yake akimuelezea M.Mungu yuko wapia jaribu kuchungulia kwenye youtube mwanzo mwisho naamini utapata vitu vizuri na imani yako itatulizana.


Nae Ustdh Khalid Mustfa kutoka Madrasat Taqwa Majengo ya juu akichukua kumbukumbu ili aweze kuwafikishia baadhi ya  waumini ambao hakuweza kufika katika muhadhara huo kama alivyo nidokeza kutokana na unyeti wa mada zinazo endelea.

Nae Ustadh Omary kutoka Patandi ambae ni mukhitimu wa Maahadi ya kisauni Nchin Kenya aliye kaa kwa mshangao katika safu ya kwanza mbele baada ya kusikia namna mawahabi wanavyo potosha umma kwa kukataa kwao Majazi na Taawili ambapo Mtume ( s.a.w ) anamuombea Swahaba wake Abdallah Ibun Abbas Mwenyezi Mungu amfahamishe Ibn Abbas Tafsir na Taawili ya aya za Qur-an ambapo mtoa mada alipo alitoa mifano mingi mpaka kufikia kuielezea aya  iliyoteremshwa Makka Sura ya 56 kuteremshwa sura yenye aya 182 matamko 860 herufi 3826 kwa mpangilo wa msahafu ni sura ya 37 aya ya 99 yenye kujilikana kwa jina la Surat Sswaaffaat M.Mungu anasema :-
 وَقَالَ إِنِّي ذَاهِبٌ إِلَى رَبِّي سَيَهْدِينِ

 "Na akasema: Hakika mimi nahama, nakwenda kwa Mola wangu Mlezi; Yeye ataniongoa "
na Mufasirina wana kubaliana kwamba hijra aliyo ifanya Nabii Ibrahima baada ya kutoka salama kwenye Moto alikwnda katika mji wa Shamu mtoa mada akasema "kwa mujibu wa mawahabi wanaokataa taawili na majazi wakichukuwa dhwahiri ya aya kwamba M.Mungu alikuwa yuko kwa maaan Nabii Ibrahimu alihamia mji wa shamu "
 إِنَّا لِلّهِ وَإِنَّـا إِلَيْهِ رَاجِعونَ
 Huu ni msiba mkubwa .
UWASUWA  wanakuahidi mwezi ujao kukuletea Muhadhara mwingine Mkubwa kushinda huu mada kuu itakuwa ni Funga ya Ramadhan je,twatakiwa kufunga kwa kufuata mwezi utakapo onekanapopote Duniani au kila watu wa mji wanakuona kwao.
Kwa sababu kuna Redio moja hapa Nchini wanasema ni yakiislamu  ikikaribia muandamo wa mwezi wa Ramadhan ina amua kusema uongo mwaka majuzi tulidanganywa kuna mwanamke Mkoa wa Mwanza yeye na familia yake tu wameuona mwezi na UWASUWA  walipo jitahidi kuwasiliana na waislamu wa Mwanza waislamu wa Mwanza walikanusha habari hizo .
        Na mwaka uliofuata tulidanganywa kuwa huko Kibiti Lindi Mwalimu wa shule na wanafunzi wake wameuona Mmwezi na tulipo lifutilia hilo kwa Masheikh wa maeneo hayo pamoja na Waumini wao walikanusha kwa nguvu zote  taarifa hizo za uzushi kwa ajili ya maslahi fulani
 UNAWEZA KUZIPATA BAADHI YA TAARIFA ZETU KUPITIA KWENYE FACEBOOK AU YOUTUBE AU MOJA KWA MOJA KUPITIA BLOG HII .






Saturday, 25 April 2015

HATIMAE SHEIKH MUSABAHA KASSIM AIBUKA KUWA SHEIKH WA MKOA WA MARA 25/4/2015

Baadhi ya masheikh kutoka Kondoa na Arusha wapongeza waislamu wa mkoa wa mara kwa kumpata shikh wa mkoa


makatibu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania( BAKWATA )Mkoa wa Mara wakiwa na baadhi ya waislamu, habari  kamili baada ya muda kidogo

Saturday, 4 April 2015

UWASUWA NA KAZI YA DA`AWA WILAYANI KARATU 3/4/2015 SIKU YA IJUMAA

Umoja wa Walimu wa Ahlis Sunna Wal jamaa Arusha ( UWASUWA ) baada ya kufanya ziyara nyngi katika Misikiti ya Wilayani Arusha ambapo ndipo Makao Makuu yake imelazimika kutoka nje ya Wilaya hiyo na kuelekea Wilayani Karatu,lengo kubwa ni kuzidi kuwaunganisha Waislmu ili kuzidi kuwa pamoja kama Qur-an inavyo tutaka "SHIKAMANENI KATIKA KAMBA YA MWENYEZI MUNGU WALA MSIFARIKIANE"Qur-an 2:103
HUU NI UPANDE WA KUSHOTO WA MSIKITI MKUU WA IJUMAA WILAYANI KARATU

 MSIKITI HUU UKO KATIKATI YA MJI WA KARATU NA UMEPAKANA NA SOKO UPANDE WAKE WA KUSHOTO
 Utadh masoud Hussein mwenye kanzu ya kijivu kutoka UWASUWA Arusha ndiye aliye wasilisha mada katika msikiti huo ambapo aliwahamasisha waislamu kutafu Elimu na kueleza changamoto nyingi ambazo waislamu wanalazimika kukabliana nazo katika zama tulizo nazo kama vile watoto wetu kukosa muda wa kutosha juu ya kujifundisha dini yao,vipindi vya dini mashuleni kukosa walimu wakutosha ,kinamama kutosoma dini pia kinababa kuto hudhuri darasa mbalimbali baada ya swala ya maghrib hali yakuwa muislamu kutafuta elimu ni jambo la lazima kwani Mtume Muhammad (S.A.W) anasema "KUTAFUTA ELIMU NI FARADHI MNOO JUU YA KILA MISLAMU WA KIUME NA WAKIKE"

IMAMU MKUU WA MSIKITI WA IJUMAA KARATU SHEIKH ABUBAKAR ALIYE VAA KILEMBA AKIWA NABAADHI YA WAUMINI WA MSIKITI HUO

MSIKITI WA IJUMAA KARATU
UWASUWA WALILAZIMIKA KUTEMBELA MSIKITI ULIO KARIBU NA MSIKITI WA KARATU MJINI, MSIKITI WA ROTYA KWA USTADH ISSA KWA LENGO HILO HILO LA KUFIKISHA DA`AWA NA KUBADILISHANA FIKRA NA WAISLMU WA MAENEO HAYO
MSIKITI WA ROTYA


NA HATIMAE ZIRA YAO ILIISHIA KATIKA MSIKITI WA MAKUYUNI KWA USTADH ALLY AMBAPO HAPO KULIKUWA NA MAULIDI YA KUZALIWA MTUME MUHAMMAD ( S.A.W )

HIKI NDICHO KINARA KAMA TUNAVYO MUONA MC AKIREKEBISHA MITAMBO

NA HUU NDIO MSIKITI MKUU WA MAKUYUNI KAMA UNAVYO ONEKANA KATIKA PICHA

BAADHI YA WAKAZI WA MAKUYUNI WAKIRUDI KUTOKA KWENYE ZAFA



Sunday, 15 February 2015

LONGUO-MOSHI WAKIADHIMISHA MAZAZI YA MTUME MUHAMMAD ( S.A.W ) LEO TAREHE 15/2/2014

HUU NDIO MSKITI WA LONGUO:- HABARI KAMILI BAADA YA MUDA KIDOGO
MSIKITI HUU IMAMU WAKE AJULIKANA KWA JINA LA SHEIHK HUSSEIN CHIFUPA

MSIKITI WA IJUMAA LONGUO ,MSKITI HUU UNAPATIKANA KATIKA MKOA WA KILIMANJARO JIRANI  NA HOSPITALI YA KCMC

 MSEMA CHOCHOTE ( MC )ALHAJ USTDH AMIR AKINONEZWA NENO BAADA YA KUSOMA RATIBA YA HADHRA HII .

MZEE SAIDI KHATIBU AKITIA FATIHA KWA AJILI YA KUANZA HADHARA HII KAMA ANAVYOONEKANA AKIWA AMESHIKA MAIKI. NA BAADA YA FATIHA HIYO MOJA KWA MOJA TULITAWASALI KWA MAJINA YA M.MUNGU

USTADH IBRAHIMU KUTOKA MBOKOM NDIO ALITUSOMEA WASILATU SHAFIY KAMA ANAVYOONEKANA AKIWA AMESHIKA KITABU.

NAYE USTADH ISSA GODA ALITAWALIA KAZI YA KUREMU NDUGU ZETU WALIO TANGULIA MBELE YA HAKI.
 
QARIU WETU KATIKA MALIDI HAYA ALIKUWA NI USTADH ADAMU, KAMA TULIVYO ZOEYA KATIKA HADHARA MBALIMBALI ZA MAULIDI KUTANGULIWA NA MANENO YA M.MUNGU( QUR-AN ).

KAZI YA UTAMBULISHO WA WAGENI ILIFANYWA NA USTADH ABDILAHI

 MC AKIPELEKA MAIKI KWENYE MADRASA YA NOOR KWA AJILI YA SWALATU ALANNABIY

MADRASAT RAAZIQYA LONGUO WAKI IMBA QASWIDA

MABANATI WA MADRASA RAAZIQIY WAKICHEZA KWA MBWEMBWE NA YOTE HAYA NIKATIKA KUMFURAHIYA  NA KUMPENDA MTUME ( S.A.W ) KAMA ALIVYOSEMA MTUME WAFUNDISHENI WATOTO WENU MAMBO MATATU :-"KUMPENDA MTUME,KUWAPENDA AHLIBAYT WA MTUME NA KUSOMA QUR-AN "


HAFLA YA MAULIDI ILIZIDI KUCHANGAMKA PALE MADRASA YA QAADIRIYYA WALIPO WALIPO PIGA QASWIDA YA YAO KAMA UNAVYO WAONA VIJANA WA MADRSA HIYO WAKIWA WAMESIMAMA WAKICHEZA


KINA MAMA WAKIWA JUU YA VITI KUTOKANA NA ENEO LETU KUWA NI DOGO



SHIA PIA HAWAKUBAKI NYUMA KATIKA MAULIDI HAYA KAMA UNAVYO WAONA WAKIIMBA QASWIDA YAO


SHARIFU ( DIWANI ) YEYE ALISIMAMIA ZOEZI LA HARAMBEE KWA AJILI YA UJENZI WA MADRASA

MGENI RASMI SHEIKH ALHAJ YUSUFU LASENGA AKIWA TOA NASAA ZAKE JUU YA KUZIDI KUMPENDA MTUME


 HAWA NI BAADHI YA WAALIKWA KWENYE MAULIDI HAYO










USTADH AKITUSOMEA MLANGO WA TATU








Sunday, 8 February 2015

SHREHE ZA MAULIDI YA MTUME MUHAMADI (S.A.W) ZAFANYIKA LEO TAREHE 8/2/2015 KATIKA MSIKITI MKUU WA NGARENARO


 
 HII NI SEHEMU YA KUINGILIA MSIKITINI UPANDE WA BARABARA KUU IENDAYO MJINI ARUSHA

IMAMU MKUU WA MSIKITI WA NGARENARO SHEIKH MAHMUUDU SALIMU NYAMBWA AKIWA NJE YA MSIKITI HUU KABLA YA HADHARA KUANZA


 BAADHI YA WANAFUNZI WAKIANZA KUINGIA MSIKITINI KWA AJILI YA KUMUADHIMISHA MTUME MUHAMMAD ( S.A.W )
USTADH ABDUL-AZIZ GAIRO AKIFUNGUA HADHARA KWA KUSOMA QUR-AN TUKUFU
 WANAFUNZI WA MADRASA WAKIANDAA DUFU ZAO KWA AJILI YA KASWIDA
MUDIYR WA AZHHAR-ARUSHA

MUDIYRU WA AL-AZHAR SHARIYF MKOA WA ARUSHA AKIWASILISHA MADA





 SHEIKH ALLY KUTOKA TAASISI YA A.B.C AKIWASILISHA MADA YAKE KAMATUTAKAVYO KULETEA HIVI PUNDE
 ENDELEA KUFUATILIA KWA KARIBU



Thursday, 5 February 2015

HISTORIA ILIYO FICHWA TANZANIA

Mtu yoyote hii leo ikiwa ataingia katika mitandao ya kijamii na kusoma mjadala unaofanyika kuhusu Mahakama ya Kadhi ni lazima atapata mshtuko mkubwa kutokana na lugha kali na wakati mwingine matusi kati ya hao wanaojadiliana. Kila upande ukitupa shutuma na maneno makali dhidi ya upande mwingine. 

Ukipitia majadiliano yote kitu kimoja kinachojitokeza wazi na dhahiri kabisa ni kuwa kuna mpasuko mkubwa kati ya Waislam na Wakristo kuhusu Mahakama ya Kadhi. Chuki na uadui sasa upo wazi bila kificho. 


Hili linawezekana vipi wakati viongozi wetu wanatuambia kuwa Baba wa Taifa alituachia misingi imara ya umoja? Wahenga wamesema dalili ya mvua ni mawingu. Suali la kujiuliza ni hili, wapi sisi kama taifa tumejikwaa? Wengi katika hao wanaojadili hiyo Mahakama ya Kadhi ukweli ni kuwa hawaijui vyema historia ya Tanzania au ukipenda Tanganyika. 


Wengi katika hawa waliojizinga katika malumbano haya baadhi ni watu wazima walio na umri zaidi ya miaka 50 na vijana ambao wamezaliwa baada ya Tanganyika kupata uhuru wake mwaka 1961. 


Mjadala unafanyika katika mazingira ya ujinga wa kutojua historia. Sasa hapa linakuja swali imekuwaje kuwa watu hawa ambao kwa sasa ndiyo wengi katika jamii yetu hii leo hawaijua historia ya nchi yao?


Vipi tumekuwa na Chuo Kikuu kwa karibu ya nusu karne na sasa vimeongezeka vingine vingi lakini hadi sasa ikawa historia yetu ni ya kubabaisha haijakaa sawa hadi leo? Mimi sitatoa jibu kwa sasa ingawa jibu ninalo. Huko vyuoni ni historia gani inasomeshwa ambayo inawafanya watu wasijijue?

Baadhi ya wachangiaji katika hiyo mitandao ya kijamii na inaelekea hao ni Wakristo wanasema iweje Mahakama ya Kadhi igharimiwe na serikali ilhali serikali hii haina dini? Waislam wanaleta jibu wakisema mbona serikali inatoa mabilioni kila mwaka kwa makanisa kuhudumia taasisi zao kupitia “Memorandum of Understanding (MoU)?” Kwa wale ambao labda hawaujui huu mkataba ni kuwa mwaka wa 1993 Serikali ya Tanzania ilitiliana sahihi mkataba na makanisa, mkataba uliokuja kujulikana kama Memorandum of Understanding. 


Makubaliano ambayo serikali iliridhia na kuidhinisha elimu, huduma za jamii na afya ziendeshwe na Christian Council of Tanzania (CCT) na Tanzania Episcopal Conference (TEC) kwa kushirikiana na serikali.


Mkataba huu ulitayarishwa na Dr. Costa Mahalu, wa Kitivo cha Sheria Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam na ukatiwa sahihi na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Edward Lowassa. Kikubwa katika mkataba huu kwanza ni ule usiri uliogubika mpango mzima na pili ni kuwa ulitiwa sahihi bila ya kuwashirikisha au kuwafahamisha Waislam. 


Ili makubaliano haya yaweze kutekelezeka, serikali ilibidi ifanye marekebisho kifungu 30 cha Education Act No. 25, 1978. Katika mabadiliko haya kuletwa Bungeni ndipo Waislam wakajua kuhusu hii MoU kati ya Serikali na Makanisa.


Suali lingine la kujiuliza ni inakuwaje jambo zito kama hili lilipitishwa na Bunge letu bila kipingamizi? Suala hili limepita kwa kuwa Waislam Bungeni waliamini kuwa uamuzi huo una maslahi na taifa letu? Au limepita kwa kuwa Waislam katika Bunge ni wachache wameelemewa na ndugu zao Wakristo kupelekea kuwa sasa hawana sauti kwa uchache wao? Ikiwa huu ndiyo ukweli wenyewe, tumefikaje hapa na nini athari ya jambo hili kwa mustakbali wa taifa letu? 


Kwa uchache unaweza mtu ukajiuliza kwa nini basi serikali hiyo hiyo haikuja na mpango wowote hata kama si sawa na ule wa Makanisa wakatoa fedha kwa taasisi za Kiislam na wao wajiletee maendeleo kama hayo ya Makanisa? Mimi sitatoa jibu ingawa majibu ninayo. 


Kwa kuhitimisha hebu tujiulize kwani Mahakama ya Kadhi ni kitu kipya katika nchi hii kiasi cha kusababisha mtafaruku huu ambao hivi sasa tunaushuhudia?


Ukweli ni kuwa ukoloni umeingia Tanganyika umekuta Waislam wakijihukumu kwa kitabu chao. Mmishionari Johan Krapf kaja Tanganyika na alipokelewa na Chifu Kimweri wa Usambaa mwaka 1848. 


Krapf alipokelewa kwa ukarimu wa hali ya juu na alimkuta Chifu Kimweri Muislam, anajua kusoma na kuandika kwa herufi za Kiarabu akihukumu katika barza yake iliyokuwa Vuga. Ni wazi kuwa Chifu Kimweri hakuwa anahukumu kutoka, “Order in Council,” kutoka India kwani Waingereza walikuwa bado hawajafika.


Chifu Kimweri alikuwa anahukumu kwa sheria kama walivyohukumiana Waislam katika ukanda wa pwani ya Afrika Mashariki kwa miaka mingi. Mimi nimekuwa na kupata fahamu katika Tanganyika ya 1950/60 na nina kumbukumbu za hizi mahakama za kadhi na baadhi ya hawa mahakimu nimewaona kwa macho yangu aidha wakiwa katika mahakama wakihukumu na wengine nimewaona mitaani na wengine nimewaona wakisuhubiana na wazee wangu. 


Namkumbuka Sheikh Abdallah Simba kutoka Songea. Nikifumba macho ni kama vile namuona Sheikh Abdallah Simba. Alikuwa kija Dar es Salaam na Land Rover yake mwenyewe na siku zote akivaa kanzu, koti na tarbush. Sheikh Abdallah Simba alikuwa na watoto wawili Bi. Habiba na Mwajuma. Bi Habiba alikuwa na umri sawa na mama yangu na alikuwa ‘’nurse’’ Princes Princess Margret Hospital (sasa Muhimbili Hospital) lakini Mwajuma yeye alikuwa makamu ya dada yangu mkubwa. 


Mwajuma akisoma St. Joseph’s Convent School (sasa Forodhani). Sheikh Abdallah Simba alikuwa akihukumu katika mahakama huko Songea kwa sheria za Kiislam na akifahamiana na babu yangu Salum Abdallah toka ujana wao katika Dar es Salaam ya 1920. 


Sheikh Abdallah Simba akiishi Songea lakini alikuwa na nyumba mbili moja Mtaa wa Kipata (sasa Mtaa wa Kleist Sykes) nyingine Mtaa wa Somali (Sasa Mtaa wa Omari Londo). Majina ya mitaa hii ilibadilishwa kuwaenzi wazee hawa Kleist Sykes na Omari Londo walioacha alama katika historia ya uhuru wa Tanganyika.


Kulikuwa na Sheikh Said Chaurembo akihukumu katika Mahakama ya Kariakoo. Sheikh Said Chaurembo alikuwa katika Kamati Ndogo ya Siasa ya TAA (TAA Political Subcommittee) mwaka 1950. Kamati hii chini ya Mufti Sheikh Hassan bin Amir ilifanya makubwa katika kujenga mazingira ya kuunda TANU mwaka 1954 na kumweka Mwalimu Nyerere katika uongozi wa kudai uhuru lakini hapa si mahali pake kuyaeleza hayo. 


Huyu Sheikh Said Chaurembo alikuwa na nduguye akiitwa Iddi Chaurembo huyu ndiye baba yake Sheikh Abdallah Chaurembo na wakati ule Sheikh Abdallah Chaurembo alikuwa mwanafunzi katika chuo cha Mufti Sheikh Hassan bin Amir. 


Sheikh Said Chaurembo ndiyo aliyekuwa na lile ghorofa maarufu Mtaa wa Msimbazi na Congo linalojulikana hadi leo kama Ghorofa la Chaurembo. 


Kwa kumalizia kuhusu hizi mahakama hapa Dar es Salaam napenda kueleza kuwa katika miaka ya 1960 baada ya uhuru Sheikh Kassim Juma alikuwa akihukumu katika Mahakama ya Kadhi Mkwajuni hadi mahakama hizo zilipovunjwa na serikali mwaka 1963. Sheikh Kassim Juma na yeye ana historia kubwa katika siasa za Waislam, BAKWATA na serikali baada ya uhuru.


Sheikh Abdallah Chaurembo akiwa msomi wa dini ya Kiislam alihusika sana katika harakati za kudai uhuru wa Tanganyika. Sheikh Abdallah Chaurembo alikuwapo katika mkutano wa TANU uliofanyika Mtaa wa Pemba usiku mmoja mwaka 1955 agenda kuu ikiwa vipi TANU itapunguza joto kali la Uislam ndani ya chama ili kupunguza ile taswira kuwa TANU ni chama cha Waislam. Jambo hili lilikuwa muhimu ili kumwezesha Mwalimu Nyerere kuongoza harakati za kudai uhuru kwa utulivu. 


Pamoja na Sheikh Abdallah Chaurembo katika mkutano ule alikuwapo Sheikh Nurdin Hussein na Rajab Diwani lakini mzungumzaji mkuu na aliyesukuma agenda hii ikakubaliwa na TANU na kutoa azimio alikuwa Mufti Sheikh Hassan bin Amir. Azimio lenyewe lilikuwa yeyote atakaeleta udini katika TANU “atatoswa.” Ningependa sana kueleza historia hii lakini nachelea itakuwa nje ya maudhui. Lakini mtu unaweza ukajiuliza vipi katika historia ya uhuru wa Tanganyika majina haya hayasikiki kutajwa? 


Haiyumkiniki hata kidogo kuwa wazalendo hawa walipigania uhuru wa Tanganyika ili waiweke kwenye madaraka serikali ambayo itakuja kuvunja misingi ya dini yao.


Tanga kulikuwa na Mahakama ya Kadhi na mahakama hii ilikuwa katika jengo la TAA Barabara ya 7 ambako Kadhi, Sheikh Ali bin Hemed Al-Buhry alihukumu jamii ya Waislam kwa kutumia sharia. 


Huyu Sheikh Ali bin Hemed Al Buhry ndiye baba yake Sheikh Mohamed Ali Al-Buhry na yeye ndiye alikuwa hakimu wa mwisho kwenye mahakama hiyo. Sheikh Mohamed Ali Al-Buhry alikuja baadae katika miaka ya 1968 kuhusika sana katika BAKWATA na kuna kisa cha kusisimua sana kati yake na serikali katika siasa za Waislam na BAKWATA lakini hapa si mahali pake kueleza makasa huu. 


Hapo Tanga kulikuwa na Liwali Abdallah Rished na mtaa aliokuwa akikaa ulipewa jina la Liwali Street kwa heshima yake. Baada ya uhuru ukaitwa Makoko Street kwa heshima ya mpigania uhuru na mwanachama shupavu wa TANU Rashid Makoko. 


Kulikuwa na Sheikh Seif Nassor Alhinawy ambae alikuwa Akida pale Tanga na akihukumu kwa sheria. (Akida Seif ndiye baba ya wachezaji mpira mashuhuri katika miaka ya 1960 hadi 1970, Hemed Seif, Marshed Seif na Rashid Seif ambao ukimtoa Marshed wote ndugu zake waliva jezi ya taifa). Kwa kuthamini taasisi hizi za Kiislam kuna mtaa Waingereza waliupa jina Akida Road (sasa Mkwakwani Road) kwa heshima ya Akida Seif Nassor. 


Katika Tanganyika Tanga ndiyo moja ya miji iliyokuwa na historia nzuri sana ya Mahakama ya Kadhi. Mwanzo wa miaka ya 1900 kulikuwa na Kadhi Omar Stambuli kisha akaja Kadhi Ali bin Hemed Al-Buhry, Liwali Abdulrahman bin Ali Diwani, Liwali Rished Abdallah, Omar Stambuli, Juma Mwindadi , Said bin Ali Al-Buhry (OBE), Mohamed bin Ali Al-Buhry. 


Masheikh hawa baadhi yao walifanya kazi ya ukadhi Tanga na wengine walikuwa Moshi, Arusha, Mwanza na kwengineko Tanganyika.


Tabora Sheikh Bilali Mshorwa alikuwa akihukumu kwa sheria mahakamani. Huyu Sheikh Bilali Mshorwa akifahamiana vizuri sana na babu yangu, Salum Abdallah pale Tabora kwani wao ndiyo walikuwa wanamji na wazee wa mjini wakati wao. Moshi kwa Wachagga alikuwapo Liwali Mussa Minjanga akihukumu Bomani. 


Liwali Mussa alikuwa akifahamiana na baba yangu na mtaa aliokuwa akiishi Liwali Mussa Minjanga toka enzi hizo za ukoloni ulikuwa ukijulikana kama Liwali Street na jina hili limebaki hivyo hadi hii leo.


Hali ilikuwa hivi Tanganyika nzima na Mahakama ya Kadhi haikupata kuwa katika agenda ya kufutwa uhuru utakapopatikana. Nini kilifanya serikali mwaka 1963 ivunje mahakama hizi? Jibu ninalo lakini sitalitoa kwa sasa.


Kuna watu wanasema ati kuwa na Mahakama ya Kadhi itavunja umoja wa taifa letu. Hapa linakuja swali kwani Tanzania huo umoja unaozungumziwa tunao hivi sasa? Mbona kumekuwa na malalamiko mengi tu kutoka kwa Waislam kuwa serikali ina udini na inawabagua? Hii ilianza kama manung’uniko ya chinichini kwa miaka mingi na mwisho ikaibuka kwa sauti kubwa kuwa nchi yetu inatawaliwa na “Mfumokristo” yaani nchi inaendeshwa kwa maslahi ya Kanisa. Mwaka wa 2012 Waislam walifanya mikutano nchi nzima wakitahadharisha kuhusu hili. Video za mikutano hii imezagaa nchi nzima na kwenye mtandao. Bahati mbaya hadi leo serikali imekuwa kimya. 


Labda mtu unaweza kujiuliza kwa nini serikali imekuwa kimya kwa shutuma nzito na za hatari kama hizi? Imekaa kimya kwa kuwa yanayosemwa na Waislam hayana ukweli na ithibati yoyote au iko kimya kwa kuwa inaogopa kulifingua Sanduku la Pandora? 


Jibu la swali hili vilevile ninalo. Nadhani msomaji wangu angalau kwa mbali umeweza kusoma angalau kwa muhtasari historia ya nchi yetu ilivyokuwa. Vipi tumejikuta katika huu uhasama tunaoushuhudia hivi sasa hii ni mada ya kujitegemea na In Sha Allah tutaizungumza.


Makala haya yameandikwa na

Mwanahistoria Mohamed Said

Copyright @ 2014 UWASUWA.

Designed by Japhary | Japhary Juma