Kongamano la Miiraji Tarehe 25/05/2014 saa 2:00 asubuhi Ukumbi wa CCM Mkoa - Arusha. More... Click Here!


Wednesday, 20 August 2014

Askari 40 kunyongwa Nigeria

Makumi ya askari wa Nigeria wanakabiliwa na adhabu ya kifo kutokana na makosa mbalimbali ukiwemo uhaini.
Mkuu wa Majeshi ya Nigeria Meja Jenerali Kenneth Minimah amesema kuwa askari hao 40 wanashikiliwa katika jimbo la Borno, kaskazini mwa nchi hiyo. Minimah amesema kuwa, askari yeyote anayekiuka sheria, lazima akabiliwe na adhabu hiyo. Amesema kuwa askari wanaohudumu katika majimbo yanayokabiliwa na machafuko nchini Nigeria, wanaweza kuhama na kuelekea majimbo mengine kwa amri ya makamanda wa jeshi.
Wakati huo huo ripoti zinasema kuwa, mahakama ya kijeshi ya Nigeria imeanza kusikiliza kesi dhidi ya askari wengine 100 wanaokabiliwa na tuhuma za kuasi amri ya jeshi kwa kukataa kusalia katika maeneo yenye machafuko nchini humo. Askari hao walipinga kubakia katika jimbo la Borno ambalo ndiyo ngome kuu ya kundi la Boko Haram na kutaka wapelekwe katika maeneo yenye amani.

MATAIFA YA KIARABU YAZINDUKA

Matifa ya kiarabu (Arab League)yameanza kupinga kuingiliwa Nchi ya Libya na matifa ya kigeni
Akijibu ombi la bunge la Libya kwa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuingilia kijeshi nchini humo ili kuwalinda raia na kukabiliana na makundi ya wanamgambo, Fadhil Muhammad, Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu amesema kuwa jumuiya hiyo haiidhinishi uingiliaji wa nchi za kigeni huko Libya na kwamba inaamini kuwa nchi za Kiarabu zenyewe zinapaswa kutatua matatizo yake ili kusiwepo na haja ya uingiliaji wa wageni. Naibu Katibu Mkuu wa Arab League ameongeza kuwa, jumuiya hiyo inatiwa wasiwasi na matukio yanayojiri huko Libya na kwamba inasikitishwa na mapigano na machafuko ya umwagaji damu yanayoendelea kati ya makundi yenye silaha nchini humo. Fadhil Muhammad amesema anatumai kwamba bunge la Libya litaweza kurejesha amani na utulivu nchini humo kwa kusaidiwa na nchi jirani na zile za Kiarabu

Tuesday, 19 August 2014

MATAIFA YA KIISLAMU YAONYWA KUHUSU HILA ZA MAREKANI

Baraza  la  ushauri  la  usala  la  nchi  ya  Iran  limeyaonya  mataifa  ya  Kiislam  duniani  kote  kuwa  macho  kutokana  na  hila  za  nchi  ya  Marekani.  
wito  huo  umetolewa  na  Dakta Ali Larijani  na  kuyataka  mataifa  ya  Kiislam  kutokukurupuka  kufuata  msingi  wa  demokrasia  wa  nchi  ya  Marekani  ambao  umekuwa  kwa  kiasi  kikubwa  ukikandamiza  mataifa  hayo  ya  kiislamu  kwa  maslahi  yake  binafsi.

Sunday, 17 August 2014

Wanigeria 85 wakombolewa kutoka Boko Haram

kuzisha hati
Vikosi vya Chad vimewakomboa Wanigeria 85 waliokuwa wametekwa nyara wiki iliyopita na wanamgambo wa kundi la Boko Haram huko kaskazini mashariki mwa Nigeria.  Afisa wa Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Taifa (NHRC) huko Maiduguri makao makuu ya Jimbo la Borno amesema kuwa, wanaume 62 na wanawake 22 wamekombolewa huku wengine 30 bado wametekewa nyara na kundi hilo.
 Agosti 20 wanamgambo wa Boko Haram walivamia kijiji cha Doron Baga katika pwani ya ziwa Chad na kuwateka nyara wanaume 100 na wanawake kadhaa. Watu wasiopungua 28 waliuawa na nyumba kadhaa kuchomwa moto katika shambulizi hilo.
Watu hao wamekombolewa baada ya msafara wa wanamgambo wa Boko Haram kusimama katika mpaka wa Chad ambapo ulitiliwa shaka

Friday, 15 August 2014

Khatami: Iran haitakubali ubeberu wa Marekani

 kuzisha hati
Khatibu wa Swala ya Ijumaa mjini Tehran amesema kuwa, madhali Marekani ingali inaendeleza uadui na viongozi wake wangali wanatoa matamshi ya kiadui dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kushirikiana na Washington hakuna maana yoyote.
Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami amesema hayo mbele ya hadhara kubwa ya waumini waliohudhuria ibada ya Swala ya Ijumaa mjini Tehran na kusisitiza kwamba, Marekani haifuatilia mazungumzo bali inachotaka ni kuwa na satua na udhibiti kwa taifa hili la Kiislamu. Khatibu wa Swala ya Ijumaa mjini Tehran amesema bayana kwamba, viongozi wa Marekani wanapaswa kuelewa kwamba, mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu na wananchi wa taifa hili katu hawatakubali ubebeberu wa Washington.
Ayatullah Khatami ameashiria kuongezeka matarajio na vikwazo vya Wamarekani katika mwenendo wa mazungumzo ya nyuklia ya hivi karibuni na kusema kuwa, viongozi wa Marekani hawaaminiki, wanatafuta visingizio na katu hawana nia ya kuyapatia ufumbuzi matatizo yaliyopo. Ameashiria pia matukio ya hivi karibuni nchini Iraq na kusisitiza juu ya udharura wa kulindwa umoja na mshikamano wa taifa hilo.
Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Ayatullah Ahmad Khatami amesema kuwa, kundi la kigaidi la Daesh ni natija ya siasa chafu za Magharibi huko Iraq.

Thursday, 14 August 2014

SHULE YA MSIKITI WA MTAMBANI YATEKETETEA NA MOTO

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiUGyITleydKdiD5FtwjFEA04yCzuxohQ0w2_8Xa18YiCAN3z3xQ0CoEKSTwrRWJBZlsEMUjRcp7nPOjgEf38gBHnPJbwoDJXz1xh8BKDJ8ha_UPVQKtd0yTS-6EqD8L-rKi5ig9AC0NbvZ/s1600/DSCF8503.jpg
MSIKITI WA MTAMBANI AMBAO JUU YAKE IKO SHULE YA MSIKITI HUO IMETEKETEA NA MOTO 

Tuesday, 12 August 2014

Umoja wa mataifa ya kiarabu wakaribisha kuteuliwa waziri mkuu mpya

Taarifa ya Habari za Ulimwengu kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW inasema
Waziri  mkuu   wa  Iraq  Nuri al-Maliki anayeondoka madarakani amewaambia  maafisa  wa  jeshi kutoingilia mzozo  wa  kisiasa  nchini  humo.
Katibu  mkuu  wa  jumuiya  ya  mataifa  ya  kiarabu  Arab League , Nabil al-Arabi  leo  ameunga  mkono  uteuzi  wa waziri  mkuu  mpya  wa  Iraq  Haidar al-Arabi  na  kujiunga na  sauti  zinazotolewa  kimataifa  kuidhinisha  kumuweka kando  waziri  mkuu  anayeondoka  madarakani  Nuri al-Maliki. Al- Maliki  ambae sera  zake  za  mtengano zimelaumiwa  kwa  kuchangia  kuchukuliwa  kwa  maeneo kadhaa  ya  ardhi  na  wapiganaji  wa  kijihadi  wa  kundi  la Dola  la  Kiislamu, amesisitiza  kuwa  ni waziri  mkuu  halali.
Wakati  huo  huo  wachunguzi  wa  haki  za  binadamu  wa Umoja  wa  Mataifa  wametoa  wito  kwa   jamii  ya kimataifa  kuchukua  hatua  za  haraka  kuepusha  mauaji ya  halaiki  dhidi  ya  jamii  ya  Wayazidi  nchini  Iraq.
Makao  makuu  ya  kanisa  katoliki linawataka  viongozi  wa dini  ya  Kiislamu  kushutumu  mauaji  ya  kinyama yanayofanywa  na  wapiganaji  wa  taifa  la  Kiislamu  dhidi ya  jamii  ya  Wakristo  na  makundi  mengine  ya wachache  nchini  Iraq.

Saturday, 9 August 2014

Hali ya usalama inayotawala nchini Iraq hivi sasa

kuzisha hati

Sisitizo la maulama kadhaa na wananchi wa miji mbalimbali ya Iraq juu ya umoja wa kisiasa na kuwekwa kando tofauti, kuahirishwa kikao cha bunge kwa ajili ya kuchaguliwa kundi kubwa zaidi la wawakilishi bungeni ambalo litakuwa na jukumu la kumteua Waziri Mkuu, hadi Jumapili ijayo, kuendelea jinai za kigaidi za kundi la Daesh kwa kushirikiana na mabaki ya utawala wa Kibaath na kuendelea mapigano kati ya jeshi na makundi ya kigaidi, ni matukio muhimu zaidi yaliyotawala hivi hivi sasa jamii ya Iraq.
Abdul Mahdi al Karbalai, mwakilishi wa Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Sistani, alimu mkubwa na marjaa wa kidini wa Waislamu wa madhehebu ya Kishia katika mkoa wa Karbala, amewataka wananchi kuimarisha umoja wao na kushirikiana na jeshi la nchi hiyo katika mapambano dhidi ya makundi ya kigaidi na kitakfiri nchini humo. Akiashiria juu ya umuhimu wa vyama vya siasa kuiunga mkono serikali na jeshi katika vita vyake dhidi ya magaidi amesema kwamba, kuna udharura wa kuweka kando tofauti za mitazamo na kuunganisha nguvu kwa ajili ya kupambana na ugaidi wa kitakfiri, hasa katika kipindi hiki ambacho kundi la Daesh limezidisha harakati zake za uharibifu na mauaji nchini humo.
Kwa upande wake, Wisam al Hardan, mkuu wa kongresi ya mwamko nchini Iraq amesema kuwa, maulama wa Kisuni wanatakiwa kuchukua hatua madhubuti katika kukabiliana na jinai za magaidi, sambamba na kutangaza kujibari kikamilifu na vitendo hivyo. Ameongeza kwa kusema kuwa, magaidi wa Daesh wanatumia kila suhula kwa ajili ya kutoa pigo kwa  Waislamu na Uislamu kwa ujumla, hivyo yeyote yule ananyamazia kimya jinai hizo, ni wajibu wake kutoa maelezo kwa hatua yake hiyo. Kabla ya hapo pia maulamaa 14 wa Kiislamu wa madhehebu ya Kisuni mjini Mosul, walikuwa wametangaza kujitenga kwao kikamilifu na vitendo vya kundi la kigaidi la Daesh mjini hapo. Kwengineko maelfu ya Waislamu katika mkoani Karbala walifanya maandamano makubwa hapo juzi Alkhamisi wakimuunga mkono Waziri Mkuu wa Iraq, Nouri al Maliki. Washiriki wa maandamano hayo walitangaza nia yao ya kutaka Nouri al Maliki achaguliwe kwa mara ya tatu kushika nafasi hiyo ya Waziri Mkuu. Wadhah Salim al Tamimi, mmoja wa waandaaji wa maandamano hayo alisema kuwa, kuna umuhimu wa muungano wa kitaifa nchini Iraq kuunda serikali chini ya uongozi wa Nouri al Maliki. Mbali na Karbala, maandamano kama hayo yameshuhudiwa pia katika mkoa wa Dhi Qar, kusini mwa Iraq, ambapo waandamanaji wametangaza kumuunga mkono waziri mkuu huyo. Hayo yanajiri wakati ambao baada ya kutofanikiwa vikao viwili vya bunge vilivyokuwa na lengo la kuchaguliwa kundi kubwa zaidi la wawakilishi bungeni, bunge hilo limeamua kuahirisha kikao hicho hadi siku ya Jumapili. Kwa mujibu wa katiba ya Iraq, mrengo huo mkubwa wenye wabunge wengi, utakuwa na juku la kumchagua waziri mkuu wa nchi hiyo.
Kwa upande wa usalama, mapigano kati ya jeshi la serikali na wanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh, yameendelea kuripotiwa katika maeneo kadhaa ya nchi hiyo. Duru za kuaminika zimeripoti kuwa karibu watoto 300 wa kabila la Yazidi wamepoteza maisha yao katika kipindi cha masaa 48 yaliyopita, kutokana na kukosa chakula na maji ya kunywa. Wakati huo huo Khadir al Mahna, mmoja wa wajumbe wa Baraza la Mwamko katika mkoa wa Diyala, mashariki mwa Iraq, amesema kuwa, kundi la Daesh mjini Baqubah na Mosul limekuwa likiwatumia watoto wadogo katika vitendo vya kigaidi. Weledi wa mambo wanaamini kuwa, kuchaguliwa waziri mkuu wa Iraq kutatoa pigo kwa makundi ya kigaidi na waungaji wao mkono wasioitakia heri nchi hiyo

Marekani yaendeleza mashambulizi Iraq


10 Agosti, 2014 - Saa 02:52 GM


Mashambulizi ya marekani

Marekani imesema kuwa imetekeleza mashambulizi zaidi kazkazini mwa Iraq dhidi ya maeneo yanayodhibitiwa na wapiganaji wa Jihad.
Taarifa kutoka Pentagon imesema kuwa ndege za Marekani pamoja na zile zisizo na rubani ziliharibu magari ya kijeshi ya wanamgambo hao likiwemo lile lilokuwa likiwashambulia raia wa Yazidi ambao wamekimbilia hifadhi katika mlima Sinjar.
Awali Rais Obama amesema kuwa kupitia washirika wake wa ulaya pamoja na wanajeshi wa Iraq watawakabili wanamgambo ambao wameuzunguka mlima huo.
Hatahivyo ameonya kuwa kampeni hiyo ya kijeshi itachukua miezi kadhaa na kwamba itachukua mda kwa jeshi la Iraq kujikusanya ili kutoa upinzani mkali dhidi ya wanamgambo hao.

Ndege za marekani zilizobeba misaada nchini Iraq
Wakati huohuo Ndege za kijeshi za Marekani na zile za Uingereza zimeendelea kuangusha misaada kwa raia waliokwama katika Mlima Sinjar nchini Iraq,ijapokuwa viongozi wa mataifa hayo mawili wamekubaliana kwamba hatua hiyo sio suluhu ya kudumu.
Wamesema kuwa lazima njia ya kuwaondoa raia hao hadi katika eneo lililo salama itafutwe ili kuzuia mauaji ya kimbari.
Mfanyikazi mmoja wa shirika la Amnesty International kazkazini mwa Iraq, Donatella Rovera ameiambia BBC kwamba maelfu ya raia kazkazini na magharibi mwa mlima huo wamefanikiwa kutoroka,lakini wengi zaidi katika eneo la kusini la mlima huo hawana mahala pa kwenda.
Amesema kuwa wale waliotoroka wako katika hali mbaya baada ya kukaa siku sita bila chakula na maji kidogo.

USA:Hatutakubali uongozi wa Khalifa Iraq


 9 Agosti, 2014 - Saa 11:37 GMT
Ndege za kijeshi za marekani
Rais Obama amesema kuwa hatakubali wapiganaji wa Kisunni kubuni taifa la kiislamu katika maeneo inayodhibiti ndani ya mataifa ya Syria na Iraq.
Obama alikuwa akizungumza katika mahojiano na gazeti la New York times baada ya marekani kutekeleza mashambulizi ya angani dhidi ya wanamgambo wa ki-suni ambayo amesema yalikuwa muhimu ili kuulinda mji wa kikurdi wa Irbil
Obama amesema kuwa marekani ina maslahi yake katika kuyazuia makundi ya wanamgmbo mbali na kusitisha mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa dini zilizo na wachache.
Wakati huohuo Rais Obama amesema kuwa hatakubali wapiganaji wa Kisunni kubuni taifa la kiislamu katika maeneo inayodhibiti ndani ya mataifa ya Syria na Iraq.
Obama alikuwa akizungumza katika mahojiano na gazeti la New York times baada ya marekani kutekeleza mashambulizi ya angani dhidi ya wanamgambo wa ki-suni ambayo amesema yalikuwa muhimu ili kuulinda mji wa kikurdi wa Irbil.
Obama amesema kuwa marekani ina maslahi yake katika kuyazuia makundi ya wanamgmbo mbali na kusitisha mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa dini zilizo na wachache.

Friday, 8 August 2014

CAR kuunda mahakama maalumu ya jinai

Serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati itaunda mahakama maalumu itakayochunguza jinai zilizofanyika katika nchi hiyo iliyoathiriwa na vita vya ndani. Mwanasheria Mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Ghislain Grésenguet amesema kuwa mahakama hiyo maalumu itachunguza na kutathmini jinai zilizofanyika nchini humo katika vita vya ndani. Amesema kamati ya wanasheria 8 inapitia nyaraka za awali za kunzishwa mahakama hiyo na itaanza shughuli zake wiki ijayo. Awali Rais Catherine Samba- Panza wa Jamhuri ya Afrika ya Kati alikuwa ameitaka Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) yenye makao yake nchini Uholanzi kushughulikia faili la jinai zilizofanyika nchini humo. Maelfu ya watu wengi wao wakiwa Waislamu wameuawa na malaki ya wengine kukimbia makazi yao katika mashambulizi ya kundi la Kikristo la Anti Balaka dhidi ya Waislamu walio wachache katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Waislamu Myanmar wangali katika hali mbaya


 Waislamu wa jamii ya Rohingya nchini Myanmar wangali wanaishi katika hali ngumu na mazingira mabaya na makumi ya maelfu miongoni mwao wanakabiliwa na uhaba wa chakula, maji na huduma za afya. Ripoti zinasema kuwa serikali ya Myanmar imeendeleza sera zake za ubaguzi dhidi ya Waislamu kwa kuzuia jumuiya za kimataifa za misaada ya kibinadamu kuingia katika maeneo ya Waislamu wa jamii ya Rohingya. Mwandishi wa Press TV anaripoti kuwa kambi za wakimbizi wa Kiislamu wa Rohingya hazina huduma za afya, maji na mahitaji mengine ya dharura na kwamba serikali ya Myanmar inabana shughuli za jumuiya za misaada ya kibinadamu kwa wakimbizi hao. Maelfu ya Waislamu wa jamii ya Rohingwa wanaounda asilimia tano ya watu wa Myanmar wameuawa na maelfu ya wengine kukimbia makazi yao kufuatia mashambulizi yanayofanywa na Mabudha wenye misimamo mikali wanaosaidiwa na jeshi la serikali. Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa Waislamu wa Rohingya wa Myanmar ni miongoni mwa jamii zilizodhulumiwa zaidi duniani.

Thursday, 7 August 2014

Anti Balaka wamekiuka makubaliano ya amani CAR'

Magaidi wa Anti-Balaka Msemaji wa Mungano wa Seleka katika Jamhuri ya Afrika ya Kati amesema kuwa, hatua ya kundi la Kikristo la Anti Balaka ya kuyaunga mkono majeshi ya Ufaransa dhidi ya wanamgambo wa Seleka inakinzana na makubaliano ya amani yaliyofikiwa hivi karibuni huko Brazzaville, Jamhuri ya Kongo. Djouma Narkoyo amesema kuwa, majeshi ya Ufaransa yakipata uungaji mkono wa Anti Balaka yalifanya mashambulio dhidi ya wanamgambo wa Seleka na kuua wapiganaji wasiopungua 50 huko kaskazini mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati. Taarifa zinasema kuwa, mapigano hayo yamejiri masaa machache tu baada ya Andre Nzapayeke Waziri Mkuu wa nchi hiyo kujiuzulu wadhifa huo. Wakati huohuo, Rais Catherine Samba –Panza wa Jamhuri ya Afrika ya Kati ameanza kufanya mazungumzo na wawakilishi wa makundi mbalimbali kwa lengo la kumteua Waziri Mkuu mpya wa serikali ya mpito. Rais Samba –Panza ameeleza matumaini yake kwamba, Waziri Mkuu mpya atachaguliwa kufikia wiki ijayo.

Tuesday, 5 August 2014

Waziri mwandamizi ajiuzulu Uingereza

Sayeeda Warsi  amejiuzulu  wadhifa  wake  wa  waziri mwandamizi  katika  wizara  ya  mambo  ya  kigeni  ya Uingereza  leo, akisema  kuwa  hawezi  tena  kuunga mkono  sera  za  serikali  hiyo  kuhusiana  na  mzozo  kati ya  Israel  na  Hamas. Warsi , amekuwa  Muislamu  wa kwanza  katika  baraza  la  mawaziri  wa  Uingereza  mwaka 2010  lakini  baadaye  alishushwa  cheo  na  kuwa  waziri mwandamizi  katika wizara  ya  mambo  ya  kigeni  na waziri  wa  masuala  ya kidini  na  jamiii.

Marekani yatoa kauli mbiu za ghiliba kwa Waafrika

Marekani yatoa kauli mbiu za ghiliba kwa Waafrika

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani John Kerry kabla ya kuanza kikao cha pamoja cha viongozi wa Afrika na Marekani mjini Washington amedai kwamba, serikali ya Washinton inashikamana kikamilifu na thamani na misingi ya demokrasia na utetezi wa haki za binadamu.
Akizungumza mbele ya wanaharakati wa jamii na makundi ya kiraia hapo jana, Kerry ametaka ziimarishwe asasi na taasisi mbalimbali barani Afrika badala ya kuimarishwa nguvu za viongozi wa Kiafrika na kusisitiza kwamba, Washington inaunga mkono ukomo wa mihula miwili ya uongozi kwa marais katika nchi za Kiafrika. John Kerry amewataka viongozi wa Kiafrika kutobadili katiba kwa ajili ya maslahi yao binafsi au ya kisiasa.
Nara na kauli mbiu za ghiliba na hadaa za uungaji mkono wa misingi ya haki za binadamu za Marekani zinatolewa na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa nchi hiyo katika hali ambayo, utawala wa Kizayuni wa Israel unaendelea kufanya mauaji na jinai za kivita na zilizo dhidi ya binadamu dhidi ya wananchi wa Palestina wa Ukanda wa Ghaza kwa kupata uungaji mkono wa moja kwa moja na misaada ya fedha na silaha ya Marekani. Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch limetangaza kuwa, mauaji dhidi ya wananchi wa Ghaza ni jinai za kivita na limetaka mashambulio ya majeshi ya Israel dhidi ya wananchi wa Ghaza yakomoshwe haraka iwezekanavyo.
Kikao cha pamoja cha siku tatu cha viongozi wa Afrika na Marekani kilianza jana mjini Washington lengo kuu likiwa ni kuimarisha uhusiano unaozidi kuyumba kati ya Marekani na nchi za Kiafrika.
       Habari hii kwa hisani ya idahaa ya kiwsahili ya redio tehran

Copyright @ 2014 UWASUWA.

Designed by Japhary | Japhary Juma